Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 5:39 am

NEWS: MCHAWI MESSI ASHINDA KWA MARA 6 BALLON D'OR

Ufaransa: Mshambuliaji wa Club ya Barcelona na Timu ya Taifa ya Argentina Leonel Adres Messi ameshinda kwa mara ya 6 tuzo ya Ballon D'or akiwabwaga washiriki wenzake Virgil van Dijk wa Liverpool na Cristiano Ronaldo wa Juventus.

Tuzo hizo zimetolewa usiku wa kuamkia leo wa Dec 2, 2019 Nchini Ufaransa.

Lionel Messi ndani ya mwaka 2019 ( mpaka sasa ) amefunga magoli 54
amefanya Assist kwenye mabao 23.
ni Mfungaji bora UEFA.
ndio Mfungaji bora La LIGA.
ndio mwenye Assist nyingi La LIGA
Ameshinda taji la Laliga, pia ameshinda taji la Supercopa kwenye timu ya taifa ya Argentina.


Pichichi trophy.
Mfungaji bora bara la ULAYA.
Mchezaji bora La LIGA
Mshambuliaji bora wa UEFA
Mchezaji bora wa kiume wa Dunia wa FIFA 2019.

Akizungumzia kutwaa kwa Messi tuzo hiyo, Van Dijk ambaye alikuwepo katika sherehe za tuzo hizo huku Ronaldo akikosekana, alisema kufanya vizuri kwa mpinzani wake kumemfanya kuwema Historia.

β€œ Nafikiri MESSI ni mchezaji bora Duniani, nafikiri MESSI anastahili kutwaa Ballon D’ Or ilmradi bado anacheza soka yeye ni Bora .

"Nina furaha kwa namna nilivyokuwa na mwaka bora. Messi ni bora katika historia? Amekuwa juu na ni kwa sababu ya kuwa ni mchezaji bora," alisema beki huyo, aliyeshika nafasi ya pili, nyuma ya Messi.

Awamu nyingine ambazo Messi ametwaa BallondOr ni 2009, 2010, 2011, 2012 na 2015. Mwaka jana tuzo hiyo, alitwaa kiungo, Luka Modric wa Real Madrid.