Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 4:28 am

NEWS: MBUNHE SELASINI AACHIA NGAZI CHADEMA BAADA YA KUONDOLEWA WHATSUP

Mbunge wa Rombo Joseph Selasin ametangaza kuachana na Chama Chake cha Chadema na kujiunga na chama cha NCCR - Mageuzi baada ya kumaliza kipindi chake cha Ubunge mwaka huu.

Selasini ametangaza uwamuzi huo leo Jumanne Aprili 28,2020 baada ya kudai kuwa chama chake kimekuwa na mwenendo wa kumtenga.

Selasini, amesema ameondolewa bila kupewa taarifa kwenye 'Group la WhatsApp' la Wabunge wa chama chake, ambalo pia yumo Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, kitendo ambacho amekichukuliwa kama ubaguzi kwa chama chake hicho.

"Kunawatu ambao niliposema nimeondolewa kwenye group la Whatsup la Wabunge walishangaa mkidogo, kundi la whatsup la wabunge ni kundi la Kazi ambalo ndani yake yupo mwenyekiti wa chama Katibu mkuu, na wengine, nitoafuti kabisa na makundi mengine ya whatsup humo mtaani kama vile ya makundi ya kidini au laharudi"- amesema Selasini.

Selasini amesema baada ya uongozi kukutoa maana yake hawataki upate habari za chama " kwamaana hiyo wewe sio mwenzao"

Aidha katika tukio lingine wakati akiendelea kutoa msimamo huo Jeshi la Polisi lilivamia mkutano huo na kuamrisha watu na waandishi waliokuwepo kutawanyika.