Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 5:39 pm

NEWS: MBUNGE WA UBUNGO KUBENEA AMJIBU MBOVU SPIKA WA BUNGE

Dar es salaam: Mbunge wa jimbo la Ubungo Saed Kubenea amesema kuwa spika aache kushughulika na vitu vidogovidogo badala yake azungumzie usalama wa Mbunge Lissu aliyepigwa risasi tarehe 7 mwezi huu, akihojiwa na Gazeti la mwanahalisi jana Kubenea amesema kuwa anamshangaa spika kubishana na mbunge kuhusu kupigwa kwa Risasi kwa Lissu "haya mambo ya idadi ya risasi kumi, ishirini sio ishu, ishu lissu anaumwa yupo hospitali mahututi,. spika wa bunge badala ya kuelezea uma juu ya nani aliyemshambulia Lissu anabishana na Mbunge kuhusu Risasi, yeye alitaka apigwe ngapi? alihoji Kubenea

Kobenea alisema kuwa yeye kama kubenea haogopi kufukuzwa bungeni kwani yeye hakuzaliwa na akiwa mbunge "huyu anazungumza nini..? sisi tunauchungu na mtu wetu kupigwa risasi, asizungumzie idadi ya risasi, na hakuna mtu anaye ogopa kufukuzwa bungeni, mi sikuzaliwa kuwa mbunge... yaani hapa mtu asinitishe kuhusu ubunge" aliongea Kubenea

Kubenea ameyasema hayo baada ya spika (Job Ndugai) kumtuhumu kuwa alikwenda kanisani kulidhalilisha bunge kwa kusema kuwa spika wa bunge alidanganya juu ya idadi ya Risasi alizopigwa mbunge Tundu Lissu, spika aliangiza kamati ya maadali kumtafuta Kubenea kokote alipo aje kuhojiwa kujibu tuhuma alizomtuhumu spika wa bunge ijumapili hii katika kanisa la Ufufuo na uzima lake mchungaji Josephat Gwajima lililopo ubungo jijini Dar es salaam.