- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE WA TUNDUMA NDEGE ZA NINI WAKATI HALI YA AFYA MBAYA NCHINI
Dodoma: MBUNGE wa Tunduma,Franka Mwakajoka (Chadema) amesema inasikitisha kuona serikali inakimbilia mabiloni ya fedha kununu ndege wakati hali ya afya ni mbaya nchini.
Mwakajoka ametoa kauli hiyo jana bungeni wakati akichangia hotuba ya bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18 katika Wizara ya Afya Maendeleo, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto.
Mbunge huyo akichangia amesema kwa sasa hali ya vituo vya afya nina hali mbaya kutokana na kukosekana na vifaa muhimu vya matibabu.
Amesea inasikitisha kuona hospitali nyingi za mikoa hazina CITY SCAN na MRI kwa ajili ya kuokoa maisha ya akina mama na watoto kwa lengo la kuboresha afya za kada hiyo.
Amesema vipimo hivyo vimekuwa vikipatikana kwa gharama kubwa jambo ambalo linaonesha zaidi kuwa serikali inafanya biashara badala ya kutoa huduma inayostahili kwa jamii.
Anashangazwa na serikali ikishindwa kutoa kipaumbele katika swala la afya na badala yake wameelekeza fedha nyingi katika ununuzi wa ndege ya Bombadia ambayo ingeweza kuwa na uwezo wa kujenga zahanati kila kanda zenye adhi ya hospitali ya Ocenroad.
Kutokana na kutokuwa na zahanati pamoja na vituo vya afya vya uhakika watanzania wengi wanakufa kwa ugonjwa wa kansa ambapo taarifa zinaonesha kuwa ifikapo 2020 watu wengi watakufa kwa kansa zaidi.
Umefika wakati sasa wa serikali kuona uwezekano wa kupunguza fedha katika maeneo ambayo hayana umuhimu na badala yake waelekeze fedha hizo katika sekta ya afya.
Aidha amesema hakuna njia yoyote ya kupunguza vifo vya akina mama na watoto kama hakuna zahanati za kutosha wala vituo vya kutosha vya afya.
Kwa sasa kuna upungufu wa hospitali 20 nchi nzima vituo vya afya upungufu ni 3913 na zahanati kuna upungufu wa zahanati 8075.