- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE WA TUNDUMA CHEDEMA AKAMATWA NA JESHI LA POLISI
Mbunge wa Tunduma (Chadema),Frank Mwakajoka amekamatwa na Jeshi la polisi mkoani songwe kwa kosa la kumpiga ofisa mtendaji wa mtaa mwaka jana 2018
Jeshi hilo limepanga kumfikisha mahakamani muda wowote kujibu tuhuma hizo za mwaka jana.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Songwe, George Kyando amedhibitisha kukamatwa kwake leo Alhamisi Julai 11, 2019 na amesema mbunge huyo amekamatwa leo na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo zinazo mkabili.
Amesema kuwa Mwakajoka anadaiwa kumpiga mwananchi ambaye hajamtaja jina, kwamba kesi hiyo ni ya muda mrefu "Kuhusu jina la mtu aliyepigwa hapa sina labda unipe muda ili nilitafute,β amesema kamanda huyo baada ya kuulizwa na mwandishi wa mwananchi
Katibu wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha) Mkoa wa Songwe, Ayub Sikagonamo amedai Mwakajoka amekamatwa kwa madai ya kumpiga ofisa mtendaji wa mtaa, Deus Mwampashe. Mbunge huyo anatarajiwa kufikishwa mahakamani leo.