Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 8:05 am

NEWS: MBUNGE WA TANZANIA AKUTWA NA CORONA

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt.Tulia Ackson amesema wamepata taarifa kuwa mmoja wa wabunge wa bunge hilo amepata maambukizi ya Corona(Covid-19) lakini anaendelea vizuri hivyo serikali inampatia matibabu stahiki, Mbunge huyo aliyeambukizwa ugonjwa huo nchini.

"Tumepata taarifa kuwa mmoja wetu amepata maambukizi ya Corona(Covid-19). Mgonjwa huyo anaendelea vizuri na serikali inaendelea kumuangalia na kumpatia matibabu stahiki, na maelezo ya mbunge huyo alisafiri kwenda Dar hivi karibuni."-Naibu Spika, Dkt. Tulia.

Huyu anakuwa ni mbunge wa kwanza kudhibitika kuwa na Virusi hivyo vya Corona nchini Tanzania na Kiongozi wa Kisiasa nchini humo.

Juzi Aprili 18, 2020 Wizara ya Afya nchini Tanzania ilitangaza kuongezeka kwa maambukizi mapya 53 na kufanya idadi ya walioambukizwa ugonjwa huo kufikia 147.

Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe mnao mwezi Machi 25 mwaka huu alitangaza hadharani kuwa amejiweka karantini kwa siku 14 siku chache baada ya kuthibitika kuwa mwanaye Dudley Mbowe amepata maambukizi ya virusi vya Corona.

Mbowe alisema amejitenga na familia yake ambayo itakuwa karantini kwa wiki mbili, na yupo nyumbani Dodoma akisubiri majibu ya vipimo ili kufahamu kama ameambukizwa Virusi hivyo ama la

Alisema tangu aonane na Dudley siku 12 zilizopita, amekutana na watu wengi hivyo ni jambo la kuomba Mungu asikutwe na corona ili aliokutana nao pia wawe salama.