Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 2:57 pm

NEWS: MBUNGE WA NYAMAGANA ATEMA POVU KWA MBUNGE LA JAMII TANZANIA.

DODOMA: MBUNGE wa Nyamagana Stanslaus Mabula amelitaka mbunge la jamii Tanzania kutumia chombo hicho vizuri ili kuibua changamoto zilizopo katika jamii.

Ameyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wabunge la jamii Tanzania kwa niaba ya Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde uliofanyika mjini Dodoma

‘’ Mimi naamini chombo hichi kimedhamilia kufanya kazivizurikama kikitumika vizurikwa mara ya kwanzamwaka huuserikaliimetenga kiasi cha fedha billion230 katika fedha hizozaidi ya billion 1 ni kwajili ya kununua dawakatika vituo vya afya na zahanati‘’ alisema.

‘’ Uwezo wetu wa kujitegemea haimaanishi tusitegemeewatuwengikutusaidia, moja ya methali kubwa ambayo aliyekuwa mfalme mwenye heshima kuwa dunianialiyewahi kuishiambayealikuwa mwanasiasa maarufu mimihuwa napenda kumwitamfalme sulemani alisema uzima na umauti vimo katika uwezo wa ulimi wote wanaopenda watakula matunda yake jawabu la upole huongeza hasira sisi tunayonia njema ya kulisaidia bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania na serikali’’alisema Mabula.

Kwa upande wake msemaji kiongozi wa bunge la jamii Tanzania na pia ni mtunza hazina

Deus Rugaila aliwaomba wananchina serikali kulipokea bunge hilo kwa mawazo chanyaili kuweza kuibua na kutatua changamoto zilizopo katika jamii.


‘’Bunge la jamii kuja kwa taifa au kwa watanzania kwanza tunaomba taifa kulipokea kwa mawazo chanya na si kwamba walipokee kwa mawazo hasi liko maalumu kwa ajili ya jamii kuibua changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii hivyo basi tunaomba ushirikiano ili kufikisha katika mamlaka husika’’ alisema Rugaila.

Nao wadau wa bunge la jamii Tanzania wakiwemo wanafunzi wa vyuo vikuu wamesema changamoto iliyokuwepo ni kubadilisha jamii kutoka katika dhana yakuacha kuwa walalamikaji,itasaidia kufikia lengo na kuleta maendeleo

Pia wameomba serikali kuwapatia usajili wa kudumu wa bunge hilo, na wameahidi kufanya kazi kwa bidii na kwakushirikiano ili kuweza kufikia Tanzania ya Viwanda

Bunge la jamii Tanzania lilianza mnamo tarehe26 mwaka 2016 ambapo lengo la kuanzishwa kwa bunge hilo ni kuibua changamoto mbalimbali na kuzifikisha katika mamlaka husika.