- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE WA NDANDA ATAKA KUMRITHI MBOWE UENYEKITI CHADEMA
Mbunge wa Ndanda kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Cecil Mwambe, ametangaza rasmi niye yake ya kutaka kugombea nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho kwa lengo la kumpokea kijiti, Mwenyekiti aliyemaliza muda wake Mbunge wa Hai Freeman Mbowe.
Mwambe ametoa adhma yake hiyo leo Novemba 26, 2019, Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza mbele ya Wandishi wa Habari, ambapo amesema kuwa licha ya kukutana na maneno ya kejeli na masimango lakini nia yake bado ni ileile na kamwe hatoweza kujitoa kugombea nafasi hiyo.
"Nimewaita kupitia kwenu nipeleke ujumbe wangu kwa wananchi wenzangu hususani Chadema juu ya adhma yangu ya kugombea na kuwa Mwenyekiti wa Chadema," amesema Cecil Mwambe
"Nilianza kuona nina haja ya kugombea baada ya kumshuhudia Mwenyekiti wa chama chetu Mh Mbowe akituambia kwamba, asingependa aendelee kuwa Mwenyekiti wetu na kwamba anatamani angeacha nafasi hiyo kwa mtu mwingine ili aendeleze yale mazuri aliyafanya, nikaona ipo haja ya kumpokea kijiti hasa baada ya kueleza kwa kina madhira ambayo amepitia kwa vipindi vilivyotangulia nikaingiwa na huruma" amesema Mwambe.
Uchaguzi wa ndani wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),unatarajiwa kufanyika Desemba 18, 2019.