- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE WA MUHEZA AMPONDA MTEULE WA RAIS
Dodoma: MBUNGE wa Muheza,Balozi Adadi Rajabu,CCM) amemponda mteule wa rais ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akiuliza swali la nyongeza kwa kutaka kujua ni kwanini serikali isione umuhimu wa kutumia sekta binafsi katika ili kuwezesha ujenzi wa reli ya Tanga-Arusha hadi Msoma.
Mbunge huyo alisema ni kwanini serikali isitumie mpango wa ppp kwa ajili ya kuwaona wawekezaji binafsi kwa lengo la kuongeza nguvu katika ujenzi wa reli ili kuharakisha zoezi hilo kwa lengo la kuokoa wakati.
Awali katika swali la msingi la mbunge huyo alitaka kujua ni lini serikali itaboresha na kujenga kisasa kwa kujenga kiwango cha Standard gauge ili iongeze uchumi na kusababisha maendeleo.
“Reli ya Tanga inategemewa sana kiuchumi kwa usafirishaji wa abiria na mizigo,aidha ni kiunganishi hadi bandari ya Tanga.
“Je nilini serikali itaiboresha na kuijenga kisasa kwa kiwango cha Standard gauge ili iongeze uchumi na kuleta maendeleo” alihoji Mbunge.
Akijibu maswali hayo Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Mhandisi Edward Ngonyani alisema serikali inakubalina na mawazo ya Mbunge ya kutumia mpango wa PPP ili kufanikisha ujenzi wa reli hiyo.
Alisema siyo rahisi kukamilisha ujenzi huo kwa kutegemea fedha za ndani hivyo kuwatafuta wafadhili ni jambo muhimu na linaliweza kurahisisha ujenzi huo.