- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE WA MTAMBILE NILINI NDOA ZA KURITHI ZITAISHA.
Dodoma: MBUNGE wa Mtambile Masoud Abdallah Saim (CUF) ameihoji serikali ina mipango gani ya kupiga marufuku tabia ya watu kurithi wajane.
Mbunge huyo ametoa hoja hiyo leo bungeni alipokuwa akiuliza swali la nyongeza kwa kutaka kujua ni hatua gani serikali inachukua kukomesha vitendo vya ndoa za kurithisha wanawake jambo ambalo linaweza kusababisha ongezeko la maambukizi ya magonjwa.
Awali katika swali la msingi la mbunge wa Lupembe,Joramu Hongali (CCM) alitaka kujua ni lini serikali itaongeza bajeti ya ujenzi,vifaa tiba na madawa katika kila kijiji na vituo vya afya kila kata.
“Waathirika wa Ukimwa katika halmashauri ya wilaya ya Njombe wamekuwa wakipoteza maisha haraka zaidi kutokana na kutembea umbali mrefu kwenda kupata huduma za matibabu.
“Je nilini Serikali itaongeza Bajeti ya ujenzi,vifaa tiba katika kila kijiji na vituo vya Afya kwa kila kata” ameihoji Hongoli.
Akijibu maswali hayo Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais-TAMISEMI,Seleman Jafo amesema serikali inaendelea kupiga vita suala la kuwepo kwa ndoa za kurithishana.
Jafo amesema halmashauri ya wilaya ya Njombe ilitengewa bajeti y ash.milioni 295 kwa mwaka wa fedha 2016/17 tayari sh.milioni 87 zilipelekwa na kuelekezwa katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya Afya.
Ameeleza kuwa kwa mwaka wa fedha 2017/18 halmashauri hiyo imetengewa bajeti y ash.milioni 435 sawa na ongezeko la asilimia 47.
Amesema kuwa serikali imeongeza fedha za mfuko wa pamoja kutoka sh.milioni 259 zilizotengwa mwaka wa fedha 2016/17 hadi shilingi milioni 306.2 kwa mwaka wa fedha sawa na ongezeko la asilimia 18.