- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: Mbunge wa Kyerwa awataka Mawaziri kuacha tabia ya kujibu maswali kwa lengo la kuwafurahisha wabunge.
Dodoma: MBUNGE wa Kyerwa Innocent Bilakwate (CCM JIMBO LA KYERWA)amewataka Mawaziri kuacha tabia ya kujibu maswali kwa lengo la kuwafurahisha wabunge badala ya kujibu kwa uhalisia wa swali lililoulizwa.
Mbunge huyo ametoa kauli hiyo bungeni wakati akuliza swali la nyongeza huku akisema anasikitishwa na majibu ya mawaziri kwani wanajibu majibu ambayo yanalenga kuwafurahisha wabunge bila kujua maswali hayo yanamanufaa kwa wapiga kura wao.
“Nasikitishwa na majibu yasiyokuwa na uhakika na majibu ya Mawaziri yasiwe yasiwe ya kuwafurahisha wabunge bali toeni majibu ya uhakika kwa faida ya wananchi” alisema mbunge huyo.
Katika swali la nyongeza mbunge huyo ametaka kujua kama serikali imetenga fedha kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi ambao wamepisha ujenzi wa barabara ya kutoka Omugakorongo-Kagarama mpaka Murongo.
Awali katika katika swali la msingi mbunge huyo ametaka kujua ni lini wananchi waliopisha ujenzi wa barabara hizo watalipwa fidia ili waendelee na mambo ya kimaendeleo na ni lini ujenzi wa barabara hiyo utaanza.
Akijibu maswali hayo Naibu wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Edwini Ngonyani amesema, majibu ya mawaziri siyo ya kuwafurahisha wabunge bali yanamaanisha utekelezaji wa shughuli za serikali.
Hata hivyo amesema kwa sasa ujenzi wa barabara hizo ambazo zimetajwa na mbunge hazijatengewa bajeti kwa ajili ya ujenzi bali upembuzi yakinifu unaendelea.
Hata hivyo amesema wale ambao wanatakiwa kulipwa fidia kwa mujibu wa sheria ya barabara Na13 ya mwaka 2007 watalipwa fidia mara zoezi la uhakiki litakapokamilika na wizara itahakikisha kuwa taratibu zote za malipo ya fidia na sheria zinafuatwa.
Aidha amesema kazi ya ujenzi wa barabara ya Omukakorongo-Kigarama –Murongo zitaanza mara baada ya usanifu wa kina kukamilika na fedha za ujenzi kupatikana.