- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE WA CCM STEPHEN MASELE AMGOMEA SPIKA NDUGAI
Dodoma: Mbunge wa Shinyanga Mjini Stephen Masele ameripotiwa kumtunushia msuli Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai baada ya Spika huyo kumtaka Mbunge huyo kurudi nchini toka jana kutokana na Utovu wa nidhamu, lakini alimgomea akisema Spika hawezi kumuita kwa kuwa ana kibali cha Waziri Mkuu (Kassimu Majaliwa).
Sasa leo bungeni Alhamisi Mei 16,2019, baada ya majibu hayo Spika Ndugai amechukua uwamuzi wa kumsimamisha kwa muda uwakilishi wake katika bunge la Afrika (PAP) hadi taarifa rasmi zitakapotolewa.
Baada ya kutangaza uwamuzi huo Spika, amemtaka mbunge huyo kurudi haraka nchini ambako pia atafikia mikononi mwa kamati za maadili za Bunge na chama chake (CCM).
Katika taarifa yake bungeni leo, Spika wa bunge Job Ndugai amesema mbunge huyo amekuwa akifanya mambo ya hovyo na kugonganisha mihimili.
"Amefanya mambo ya utovu wa nidhamu huko na taarifa tumezipata na hata kwenye mitandao imeonekana, sasa tumemtaka arudi lakini amegoma hivyo nimemwandikia barua Raid wa PAP kusimamisha kwa muda ubunge mheshimiwa huyu hadi tutakapotoa taarifa nyingine," amesema Ndugai.