Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 9:26 am

NEWS: MBUNGE WA CCM AIPINGA SEREKALI UJENZI WA BARARA ARUSHA MARA

Dodoma. Mbunge wa Serengeti (CCM) Marwa Chacha ameyapinga vikali majibu ya Serikali ya Tanzania juu ya ujenzi wa barabara inayounganisha mikoa ya Arusha na Mara.

Image result for Marwa Chacha

Katika swali la msingi Marwa alilouliza leo Jumatano Juni 26,2019 kuwa Serikali ina mpango gani dhidi ya ukamilishaji wa barabara hiyo na lini wananchi waliofanyiwa tathimini watalipwa fidia zao.

Akijibu maswali hayo kwa pamoja, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Elias Kwandikwa amekiri barabara hiyo kuchelewa kukamilika tangu ilipoanza kujengwa mwaka 2013.

Naibu Waziri amesema zipo sababu mbalimbali zilizopelekea barabara hiyo kutokamilika kwa wakati ambapo serikali imeshachukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha barabara hiyo inakamilika mapema. Kuhusu fidia kwa wananchi amesema watu 8 wameshalipwa Sh 12.87 Milioni wakati wengine 433 wamelipwa fidia ya Sh2.6 bilioni katika eneo la Makutano- Sanzate yenye kilomita 50.