- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE WA ARUSHA GODBLESS LEMA ACHILIWA HURU KWA DHAMANA
Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema hatimaye ameachiwa huru kwa dhamana leo, Marchi 5, 2020 mara baada ya kushikiliwa na Jeshi la polisi Mkoani Singida kwa siku 3.
Lema alikamatwa na Polisi siku ya Jumatatu Machi 2, 2020 baada ya Kudaiwa kutaja orodha ya watu 14 waliouawa Manyoni kwa kuchinjwa na kuchomwa moto.
Tarifa ya Chama cha Lema CHADEMA killisema jana kuwa kimeamua kuchukua hatua za kisheria ili kuhakikisha Lema anapata haki zake, kuachiwa huru kwa dhamana au kufikishwa Mahakamani, hivyo ilifungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma.
Lema alienda kuripoti Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Polisi (RCO) Arusha kama alivyotakiwa kufanya baada ya kupigiwa simu na Polisi ambao walienda kwake na kumkosa.
''Nimepata taarifa kuwa gari mbili za Polisi zikiwa na askari kanzu zime kwenda kunitafuta nyumbani kwangu bila taarifa,wamenikuta nimeondoka,hivyo nimepigiwa simu na kutakiwa ofisi ya RCO Arusha.Hawajataka kusema wana nitafutia nini?nina wasiliana na Wakili wangu kuelekea." alisema Lema kabla ya kukamatwa
"Nimefika ofisi ya RCO Arusha nikiwa niko na Viongozi wa Chama Mkoa,Wilaya,Kanda.Ofisi ya RCO haina taarifa na wito huu,isipokuwa OC CID,ninaweza kupelekwa Singida,ieleweke siwezi kujirusha kwenye gari,kunywa sumu,kujinyonga.Isije ikatokea kama kilicho mkuta mwimbaji wa Rwanda."
Baada ya hapo alisafirishwa kwenda Kituo Kikuu cha Polisi Singida ambapo alihojiwa akituhumiwa kutoa taarifa za upotoshaji zenye lengo la kuchonganisha Jeshi hilo na Wananchi.
Aidha, Katibu wa CHADEMA Wilaya Singida Mjini, alisema Lema alimwambia kuwa kosa analodaiwa kutenda ni kutaja orodha ya watu 14 waliouawa Manyoni kwa kuchinjwa na kuchomwa moto.