- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE TOWFIQ AWAASA WAHITIMU KUTODANGANYIKA.
DODOMA: Mbunge wa viti maalum Fatma Towfiq amewaasa wahitimu wa darasa la saba katika shule ya msingi ya Isungha kutodanganyika na mambo yasiyokuwa na maana kwa kuwa safari ya masomo ndio kwanza imeanza.
Mbunge Towfiq amesema hayo agosti 30 akiwa mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliyofanyika shuleni hapo wilayani Bahi mkoani Dodoma.
"Safari ya masomo ndio kwanza imeanza, msidanganyike, watoto wa kiume siku hizi kuna utamaduni wa kuiga na kujikuta mnaingia kwenye mapenzi ya jinsia moja, "alisema Towfiq.
Amewataka wazazi na walezi kuwa karibu na watoto ili kujua mienendo na changamoto zao zinazowakabili.
"Dodoma ni miongoni mwa mikoa 5 inayoongoza kuwa na tatizo la mimba za utotoni, tushikamane ili kuhakikisha jambo hili tunalikomesha ikiwemo na ukeketaji, "alisisitiza mbunge huyo.
Kwa miaka miwili mfululizo shule hiyo imeongoza kiwilaya kwa kuwa wakwanza katika matokeo ya darasa la saba ambapo jumla ya wanafunzi 103 wanahitimu mwaka huu.