Home | Terms & Conditions | Help

November 26, 2024, 9:42 pm

NEWS: MBUNGE TOUFIQ AWATAKA WANANFUNZI KUACHANA NA MITANDAO YA KIJAMII.

MEMBE: Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Dodoma Fatuma Toufiq amewataka wanafunzi kutokujihusisha na mitandao ya kijamii na badala yake wasome kwa biidi ili waweze kufikia malengo yao ya baadae.

Akizungumza wakati wa sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule ya sekondari Membe Wilaya ya Chamwino Mkoani hapailiyofanyika machi 30 shuleni hapo amesema mitandao ya kijamiihasa kwa wanafunzi wa kiumeni chanzo kinachopelea kushamiri kwa mapenzi ya jinsia moja na kusababisha kupungua kwa kiwango cha ufaulu.

Pia amewataka wazazi,walenzi na walimu kuhakikisha wanawasimamia ipasavyo watoto wao katika masomo ili waweze kuleta kufaulu ulio bora.

Awali Mkuu wa shule hiyo Deograsius Mahundi amesema zipochangamoto zinazoikabili shule hiyo ikiwemouhaba wamadawati.

Mchungaji wa kanisa la angalikana Membe Wilson Ndahaniamewaasawanafunzi hao kushika sana elimu katika maisha yako kwakuwa ni mwanga wa mafanikio.

Shule ya Sekondari Membe iliyopo Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma ilianzishwa mwaka 2009 na inajumla ya wanafunzi 200.