Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 1:16 am

NEWS: MBUNGE TOUFIQ ATOA SOMO KWA WANAWAKE.

CHAMWINO DODOMA: Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Dodoma Fatma Toufiq amewataka wanawake kutokuwa wanyonge katika kupambana na kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyoendelea katika jamii.

Kauli ya Mbunge huyo imekuja baada ya kuonekana Kata ya Mvumi Misheni Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma kuwa na wimbi kubwa la wanaume kutekeleza familia zao na manyanyaso katika ndoa hali inayopelekea watoto wengi kulelewa nawamama.

Akizungumza wakati wa sherehe za kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani Wilayani hapo Mbunge Toufiq amewataka wanawake kujitambua, kuwa jasiri ili kuweza kutokomeza changamoto hizo.

Pia amewataka wazazi kuwa karibu na watoto wao ikiwemo kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni ili kuweza kuongeza ufaulu mashuleni.

Mbali na hayo Mbunge huyo Amesema kwa mujibu wa Takwimu za Dunia zinaonyesha Tanzania ni miongoni mwa nchi 20 zenye tatizo la mimba na ndoa za utoto na katika Afrika ni miongoni mwa Nchi kumi na kuongeza kuwa Dodoma ni yatano kati ya Mikoani 26 ya Tanzania ya mwanzo yenye statizo hilo.

Akibanisha Changamoto zinazowakabili Wanawake wa Wilaya ya Chamwino wakati akisoma Risala Evaline Mremi amesema wanaume kutelekeza familia na Manyanyaso katika ndoa ni miongoni mwangamoto zinazowakabili na kusababisha ndoa nyingi kuvunjika kwa wale wasio na maamuzi ya haraka kwa kuhofia kutesa watoto wao.

Aidha wanawake hao wameiomba Serikali kuwashughulikia kisheria na badala yake kesi hizo zisiishiye polisi kwa usuluhishi Watuhumiwa watakaobanika wamefanya vitendo hivyo na kuongeza kwa kusema kutokana na familia nyingi kutelekezwa na wanaume na wanawake kuwa walezi wakuu wamemtaka Mbunge huyo kuishauri serikali ya Wilaya kuongeza kasi ya utoaji wa mikopo kwa vikundi vya wajasiliamali kwani ni ukombozi kwa familia nyingi.

Awali Diwani wa vitu maalumu Tarafa ya Mvumi Rose Jeremiah amewataka wanawake kuwajali na kuwaombea watoto yatima, kutoa elimu kwa wanawake kuhusu swala nzima la ugonjwa wa Ukumwi, kuhamasisha wanawake kujiunga na vikundi vya ujasiriamali na kutoa taarifa kwa wazazi wanaoficha watoto wenye ulemavu kuweza kupata elimu.

Siku ya wanawake Dunia kufanyika kila mwaka marchi nane ambapo kwa mwaka huu itafanyika Mkoani Dodoma Lengo ikiwa ni Chochea Mabadiliko Kuleta Usawa wa Kijinsia, Haki ya wanawake kushiriki katika maisha ya kisiasa Kauli Mbiu Ya Mwaka Huu Katika Maadhisho hayo ’badili Fikra kufikia Usawa Wa Kijinsia Kwa Maendeleo Endelevu’’.