- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE SINGIDA AHOJI WAWEKEZAJI SINGIDA
DODOMA: MBUNGE wa Singida Mjini Mussa Sima(CCM) amehoji ni lini Serikali itapeleka Wawekezaji kutokana na Mkoa wa Singida kutenga maeneo kwa ajili ya Uwekezaji.
Akiuliza swali jana bungeni mSima alidai kuwa Singida Mjini ni mji unaokuwa kwa kasi na wametenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji hivyo akahoji ni lini Serikali iko tayari kupeleka wawekezaji?
Akijibu swali hilo Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji,Charles Mwijage amesema uhamasishaji wa uvutaji wa uwekezaji ni jukumu la msingi la serikali na katika mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano wa mwaka 2016-2017,2020-2021 imeeleza walengo ya serikali.
Amesema malengo hayo ni kuongeza kasi ya kuvutia uwekezaji wa ndani na wan je katika sekta zenye tija kwa Taifa.
‘’Hivyo Wizara yangu imekuwa ikihamasisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kuja kuwekeza nchini ikijumuisha mkoa wa Singida’’alisema
Alisema moja ya kivutio ch msingi cha uwekezaji ni uwezo wa maeneo ya uwekezaji hivyo serikali imeendelea kuhamasisha Mamlaka za serikali za mitaa kupitia Mikoa na Wilaya kutenga maeneo kwa ajili ya uwekezaji.
‘’Kutokana na juhudi hizo hadi kufikia Aprili mwaka huu jumla ya mikoa 13 imewasilisha taarifa ya utengaji maeneo katika mikoa yao,napenda kuchukua fursa hii kuupongeza Mkoa wa Singida kwa kuitikia wito na tayari wametenga eneo la Hekta 6,595.6’’amesema
Mwijage alisema kutokana na jitihada hizo katika kipindi cha kuanzia 1996 hadi Aprili 2017 serikali kupitia kituo cha uwekezaji Tanzania imefanikiwa kuandikisha miradi 33 kwa Mkoa wa Singida yenye thamani ya Dola za Marekani 997.879 milioni.
Amesema ilitarajia kuajiri watu 4,344 kwa muhtasari wa kazi iliyofanyika katika kuhamasisha uwekezaji Mkoani Singida.
‘’Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na wananchi wa Singida kuwa serikali itaendelea kuvutia wawekezaji kuwekeza Mkoani Singida’’amesema