- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE PENEZA AMTAKA RAIS MAGUFULI KUKUBALI MARIDHIANO
Dodoma. Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Upendo Peneza amemuomba Rais wa Tanzania, John Magufuli kukubali kukutana na viongozi wa vyama vya siasa na Mashirika yasiyo ya Kiserekali kujadiliana kuhusu maridhiano kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba, 2020 ili kuliweka taifa kwenye hali ya Amani na Usalama.
Ameeleza hayo bungeni mjini Dodoma leo Jumatano Januari 5, 2020 katika mjadala wa taarifa za kamati za Bunge za Utawala na Serikali za mtaa, Katiba na Sheria pamoja na Sheria ndogo.
“Nichukue nafasi hii kutoa shukrani zangu za pekee kwa Rais wa Tanzania kwa kauli kuwa uchaguzi mwaka 2020 utakuwa wa uhuru na haki,” amesema Upendo.
Upendo ameomba Serikali kufanya mabadiliko katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kwa kuwaondoa wakurugenzi waliopo ili kuwe na uchaguzi wa haki na uhuru.
Upendo amesema aliunga mkono kauli ya mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe kuhusu ombi lake la kutaka yawepo maridhiano ya kitaifa ili kuondoa changamoto zilizopo. Amesema mwenyekiti huyo juzi ameonyesha nia ya kufikia maridhiano kwa kuandika barua kwa Rais Magufuli kuomba kukutana ili kuzungumza mambo mbalimbali.
“Lakini yeye (Mbowe) ametumia busara kuwa sasa wazungumze kabla ya maafa hayajatokea. Kwa busara hiyo namuomba mheshimiwa Rais atumie busara hiyo tukae chini tuzungumze twende mbele tufanye uchaguzi wa haki ili Amani tunayohitaji iweze kudumu ,”amesema