- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE MTATURU AJA NA KAULI MBIU, MANENO KIDOGO, KAZI ZAIDI, HAPA KAZI TU! !!
SINGIDA: Wakazi wa Jimbo la Singida Mashariki lililopo wilaya ya Ikungi,wamejitokeza kwa wingi kumlaki mbunge wao Miraji Mtaturu aliyewasili na kufanya mikutano kwa mara ya kwanza tangu aapishwe.
Mtaturu aliapishwa septemba 3 mwaka huu bungeni baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo Tundu Lissu(CHADEMA)kupoteza ubunge kwa kutohudhuria vikao bila ya taarifa na kutojaza fomu za tamko la mali na madeni.
Akizungumza katika mikutano aliyoifanya katika kijiji cha Mkiwa,Issuna na Ikungi Mtaturu akiwa ameambatana na Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameahidi kufanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo.
“Katika utumishi wangu mimi ni kazi tu,na serikali yetu inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi CCM inawapenda na kuwajali sana,nitahakikisha tunashirikiana pamoja ili kusukuma mbele gurudumu letu la maendeleo,na katika hii nimekuja na kauli mbiu isemayo,Maneno kidogo,kazi zaidi,hapa kazi tu,”alisema Mtaturu.
Ametumia mikutano hiyo kuweka bayana vipaumbele vyake atakavyovitekeleza katika kipindi cha ubunge wake kuwa ni elimu ambapo atahamasisha jamii kuunga mkono elimu bila malipo pamoja na kuboresha mazingira ya kufundishia.
“Jamii iliyoelimika ndio yenye uwezo wa kujiletea maendeleo, hata nilipokuwa mkuu wa wilaya nilifanyakazi hiyo, Sasa nitaendelea kuhamasisha jamii yetu kusomesha watoto,nitaunga mkono elimu bila malipo kwa kukabiliana na upungufu ya vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, walimu na ujenzi wa mabweni ili kuokoa watoto wakike kutopata mimba wakiwa shuleni,
“Katika sekta ya elimu nitahakikisha pia kila mwaka nasaidia wanafunzi 200 ambao wazazi wao hawana uwezo kwa kuwanunulia sare za shule,hapa ni wanafunzi 100 wa shule za msingi na 100 wa sekondari,nitaomba watendaji wetu wanisaidie katika kuwatambua,nafanya hivi ili kumuunga mkono Rais wetu dk John Magufuli,”alisema Mtaturu.
Pia nitawalipia ada wanafunzi 10 waliofaulu kujiunga na kidato cha tano katika shule zetu za serikali,watano wa kike na watano wakiume, “hili nilishaanza nikiwa mkuu wa wilaya kuna mtoto alipata daraja la pili kachaguliwa kuendelea na masomo wazazi hawana uwezo,nikamsaidia kumlipia helana mahitaji yake yote karibu laki 7 sasa hivi yupo shule,”alisema mbunge huyo.
Vipaumbele vingine alivyotaja ni kwenye[i] sekta ya maji,afya,kuwainua wananchi kiuchumi kwa kuhamasisha kilimo cha kisasa badala ya kile cha mazoea na kuanzisha mradi wa kukopesha wananchi ng’ombe wa maziwa utakaojulikana kama Kopa ng’ombe lipa ng’ombe ambao watasambazwa kwenye tarafa mbili.
Ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais dk Magufuli kwa kuwapelekea sh bil mbili za ujenzi wa Chuo Cha Ufundi Stadi (VETA)kama alivyoomba akiwa mkuu wa wilaya ya Ikungi.
KISHINDO CHAKE JIMBONI CHAZOA WAPINZANI 13.
Jumla ya viongozi na wanachama 13 wa vyama vya upinzani kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) na Cha Cha Wananchi(CUF) wamehama vyama vyao na kuhamia CCM.
Miongoni mwa wanachama hao yupo Katibu wa CUF wilaya ya Ikungi Selemani Ntandu aliyekuwa katibu wa kuratibu shughuli za Lissu tangu 2007, mwenyekiti wa CHADEMA katika kijiji cha Ighuka Venance Elias na Katibu wa Chama hicho kata ya Ikungi Zakaria Kadagaa.
Akikabidhi kadi kwa wanachama hao wapya Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa amewataka wanachama hao kuwa waaminifu na watiiifu kulingana na kiapo cha ahadi ya mwanachama.
Akizungumza mmoja wa wanachama waliohamia CCM Ntandu amesema huo ni mwanzo tu lakini shughuli kama hiyo itaendelea.
“Mimi ndio nilikuwa katibu wa kuratibu shughuli zote za Lissu tangu Julai mosi 2007 mpaka anapata ubunge kesi inaenda mahakamani nilisimama saa tano kumtetea nikiwa kama shahidi wake,sasa naomba nimtumie salamu huko huko kuwa akitoka Ubelgiji arudi CCM,”alisema Ntandu.
AWESO AKOSHWA NA MTATURU AMWAGA MISEMO NA KUAHIDI MAJI.
Naibu Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameahidi kupeleka maji kama Rais John Magufuli alivyoahidi wakati akizindua mfumo wa Rada ya kuongozea ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa(JNIA)jijini Dar-es-salaam.
“Huyu mbunge wenu siku ya kwanza tu kaniuliza swali la maji,unajua kwa nini,waswahili wanasema anayelala na mgonjwa ndie anayejua mihemo yake,huyu anajua shida za baba na mama zake kukosa maji,mpeni ushirikiano,
“Mtaturu kaka yangu usiogope maneno,maneno yao yaone kama maji kwenye mgongo wa bata halowani,walisema hutoshinda leo umeshinda ,walisema hutoapishwa leo umeapishwa,ukisoma tezi za rohoni zinasema adui akiniudhi nami nikisumbuka Mungu huvigeuza vyote kuwa baraka,sasa matusi waliyokutukana baraka yake Rais ametuagiza tulete maji,”aliongeza Aweso.