Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 7:41 am

NEWS: MBUNGE MTATURU AFUNGA KAMPENI SINGIDA MASHARIKI KWA KISHINDO.

SINGIDA: Mbunge wa Singida Mashariki Mhe Miraji Mtaturu novemba 23 amefunga kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa huku akiwataka wagombea watakaochaguliwa kwenda kutenda haki kwa wananchi wote bila kujali tofauti ya vyama vyao.


Akifunga kampeni katika kata za Dung'unyi,Isuna na Ikungi Mhe Mtaturu amesema wananchi wana imani kubwa na Chama cha Mapinduzi(CCM) na Serikali ya awamu ya tano Chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli na ni matarajio yao wagombea watashinda kwa kishindo.


Amesema CCM ndio chama pekee chenye dhamira na mipango ya kuwaletea maendeleo wananchi hivyo wanapaswa kuwa makini na viongozi wanaoenda kuwachagua.


"Serikali za mitaa ndio chimbuko la kuanzisha ajenda zote za maendeleo kwa hiyo sio uchaguzi wa kubeza ndio maana CCM tulijipanga kufuata mwongozo wa uchaguzi uliotolewa na wasimamizi wa uchaguzi ikiwemo ujazaji wa fomu kwa wagombea wetu wote na ndio maana wagombea wetu wote waliteuliwa na Wasimamizi wa uchaguzi,


"Wananchi mnaposhiriki uchaguzi huu mjue mnachagua maisha yenu ya kila siku kwa hiyo ukisikia kuna vyama vimejitoa kushiriki uchaguzi ujue hawana dhamira ya kweli ya kuwahudumia wananchi, na wakisema wana uchungu na maendeleo ya wananchi ni unafki wenye kiwango cha juu,"aliongeza Mhe Mtaturu.


Amesema vyama vya upinzani wanachohangaikia ni matumbo yao sio matatizo ya wananchi hivyo wajitokeze kwa wingi kwenda kuchagua viongozi bora wanaotokana na CCM.

"Hoja ya kusema tufute vyama vingi mi nasema vitajifuta vyenyewe kwa kukosa ajenda kwani tumejipanga vizuri kuwaletea wananchi

maendeleo ya kweli na sio vinginevyo,

"Tukisema CHADEMA hawajajipanga ujue ni kweli ratiba ya uchaguzi wa Serikali za mitaa walikuwanayo ila wameona sio wa muhimu,wanapambana kufanya uchaguzi wao ndani ya chama ili wagombanie ruzuku ya chama,tukisema ni Saccos ya watu wachache hatuwaonei kabisa ni ukweli unadhihirika wenyewe,"alisema Mhe Mtaturu.


Mhe Mtaturu amewapongeza wagombea wa CCM waliopita bila kupigwa kwenye vijiji vyote 50 vya Singida Mashariki na vitongoji 275 kati ya 285.

Katika mikutano hiyo katibu Mwenezi wa Chama Cha Demokrasia(CHADEMA)ambae alipewa jukumu la kusimamia ujazaji wa fomu za wagombea wa chama hicho Kata ya Dung'unyi Joselin Happe na

aliyekuwa mgombea wa Kitongoji Cha Mpipiti kupitia chama hicho John Mussa

wameamua kurejesha kadi zao na kujiunga na CCM.

Happe amekiri kuwa kulikuwa na kazi sana ya kuwaelekeza wagombea wa CHADEMA kujaza fomu kwa kuwa wengi wao hawajui kusoma na wanahitaji kupelekwa madarasa ya watu wa wazima MEMKWA.

"Kutokana na sababu hizi hawakuonewa kuenguliwa kwani fomu zilikuwa na makosa mengi sana,"alisema Happe.

Katibu mwenezi wilaya Pius Sankha ameeleza kuwa CCM imejipanga kushinda kwa kishindo katika wilaya nzima ya Ikungi yenye vijiji 101 Na vitongoji 538.

Katika jimbo Singida Mashariki uchaguzi unafanyika katika vitongoji 10 na Wajumbe wa serikali ya vijiji 7.