- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE KOMU WA CHADEMA ATIMKIA NCCR MAGEUZI
Dar es Salaam. Mbunge wa Moshi Vijijini kupitia chama cha Chadema, Anthony Komu ametangaza hii leo Machi 29, 2020 rasmi kujivua uanachama wa chama hicho na Kujiunga na NCCR Mageuzi kwa kile alichodai tabia za baadhi ya wanachama wenzake kumkatisha tamaa kwa tuhuma za usaliti zinazomkabili kwa muda mrefu.
Lakini ameahidi kuondoka katika chama hicho mara tu baada ya kumaliza muda wake wa ubunge kwa kuwa bado atahitaji ushirikiano wa chama hicho jimboni kabla ya kumaliza muda wake.
Uwamuzi huo wa Komu ameutoa leo Machi 29, 2020 jijini Dar es salaam, wakati akizungumza na waandishi wa Habari, Komu amesema amechukua uamuzi huo baada ya kusikitishwa na uongozi wa chama hicho kutosahihisha au kufafanua tuhuma za usaliti zilizosababisha mbengu ya chuki kukomaa ndani ya chama.
"Nimeomba kukutana nanyi(wanahabari) ili kuweka bayana mwelekeo wangu wa kisiasa, kwa sababu ya mijadala ya muda mrefu juu ya mwelekeo wangu wa baadaye," amesema Komu.
Komu anakuwa mbunge wa tisa kati ya 35 waliojivua uanachama kwa madai mbalimbali ya kukosekana kwa demokrasia ndani ya chama au kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli.
Licha ya kukiri kutofautiana na viongozi wenzake, lakini tofauti za kimitazamo zimemfanya aonekane muasi.
"Hatua hiyo ilisababisha kutoaminika hata pale ambapo ningeweza kutoa mchango wangu katika ujenzi wa chama chetu," amesema Komu aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Fedha wa Chadema.
Komu ametaja baadhi ya visa na tuhuma za usaliti alizokutana nazo licha ya kuwa mstari wa mbele katika hatua na matukio mbalimbali yaliyokijenga chama hicho hadi sasa.
Baadhi ya madai aliyoshambuliwa na wanachama wenzake ni pamoja na kupanga njama za kumuua Tundu Lissu, kwa kushirikiana na mtanzania aliyempokea Ubelgiji kwa matibabu.
Katika hotuba yake iliyotanguliwa na tahadhali za maambukizi ya virusi vya corona(COVID 19) nchini, Komu ameeleza namna alivyoshiriki kujenga mfumo wa siasa za vyama vingi nchini, akiimarisha upinzani kupitia NCCR Mageuzi kabla ya kuhamia Chadema.
"Msimamo huu naomba upokelewe kwa mtazamo chanya Chadema, utasaidia kuondoa majungu yanayoendelea, eti nataka nihakikishiwe kurudi nafasi ya ukurugenzi wa fedha, kurudi jimboni, eti kupindua nafasi ya mwenyekiti wetu," amesema Komu.