- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE ATOKWA CHOZI AKICHANGIA HOJA.
Dodoma: Mbunge wa Viti Maalum Faida Mohammed Bakari (CCM) amejikuta akishindwa kuchangia na akitokwa na chozi wakati wa kuchangia hotuba ya bajeti ya Wizara Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kwa kile alichosema kuwa watoto wengi wananyanyaswa.
Akichangia hotuba hiyo amesema kwa sasa unyanyasaji kwa watoto wa dogo hususani wa kike umechukua nafasi kubwa jambo ambalo linatia simamzi zaidi katika jamii ya kitanzania na kulitia aibu taifa.
Mbunge huo alichangia laiwashukia akina baba kwa maelezo kuwa wamekuwa na roho ya ukatili juu ya watoto wadodo kiasi kwamba wamekuwa wakiwaingilia watoto hao kinyime na maumbile na hata wale abao hawaingiliwi kinyume na maumbile wamekuwa wakiharibiwa maumbile yao.
“Jamani akina baba jiangalieni sana badilikeni, hii tabia ya kutembea na vitoto vidogo na wakati mwingine kufikia hatua ya kuwaingilia kinyume na maumbile ni laama acheni kabisa tabia hiyo pia wapo watu wengine ambao wanfikia hatua ya kutembea na watoto wao acheni kabisa.
“Hii ni laana nchi yetu mnaitia aibu hacheni unyanyasaji wa aina hiyo waoneni watoto hao kuwa ni watoto wenu walindeni maana vitendo hivyo ni vya unyanyasaji mkubwa” alisema Faida huku akitokwa na chozi.
Katika hatua nyingingine mbunge huyo ametangaza kuondoa shilingi katika mshahara wa waziri kama hatatoa ufafanuzi juu ya kuanzishwa kwa benki ya wananwake visiwani Zanzibar.
Naye mbunge wa Mpanda mjini,Sebastiani Kapufi (CCM) akichangia hotuba hiyo amesema Tanzania haiwezi kufikia uchumi wa viwanda kama watanzania hawatakuwa na afya njema.
Amesema kwa sasa kuna changamoto nyingi katika sekta ya afya samabamba na kukosekana na magari ya kubebea wagonjwa pamoja na kukosekana kwa mashine muhimu za kutolea vipimo vya matibabu.
Kwa upande wake mbunge wa Viti Maalim Martha Umbulla (CCM) akichangia katika hotuba hiyo ya makadirio ya mapato na matumizi katika mwaka wa fedha 2017/18 alisema katika wilaya ya Kiteto na Simanjiro, kuna tatizo kubwa la ukosefu wa magari ya kubebea wagonjwa.
Katika mjadala huo naye naye mbunge wa Viti Maalum,Suzan Ngonokulima (Chadema)amesema serikali bado haijaweka utaratibu mzuri wa kuwahudumia akina mama wajawazito ambao ni jamii ya watu wenye ulemavu.
Mbali na kutoweka utaratibu kwa akima mama wajawazito wenye ulemavu alieleza kuwa serikali imekuwa ikifanya mizaa na afya za wazee kwani hadi sasa hakuna utaratibu mzuri wa kuwahudumia wazee hao.
“Serikali imekuwa ikijitapa kuwa inawajali wazee lakini ukweli ni kwamba bado hakuna guduma madhubuti ambazo wanazitoa kwa wazee hivyo Waziri unatakiwa kueleza mpaka sasa ni mikakati gani ya kuwawezesha wazee kutibiwa magonjwa yote yanayowasumbua badala ya kuwapatia panado tu” alihoji Ngonokulima.
Naye mbunge wa Liwale,Zuber Kuchauka (CUF) ameitaka Wizara Afya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto kutatua migogoro na unyanyasaji unaoendelea katika hospitali ya magonjwa ya akili ya Milembe iliyopo mjini Dodoma.
Wafanyakazi wa ambao ni madaktari na manesi wanaofanya kazi katika hospitali ya Milembe wanafanya kazi zao katika mazingira magumu zaidi kutokana na kuwepo kwa unyanyasi wa hali ya juu ambao unafanywa na Mkurugenzi wa Hospitali hiyo.
Mbali na hilo amesema kumeghubikwa na vitendo hatari vya Rishwa na unyanyasaji jambo ambalo ni hatari kwa watumishi wa serikali katika hospitali hiyo.
Aidha aliitaka serikali kupitia Wizara husika kuhakikisha inafanya kila liwezekanalo kulipa madeni ya watumishi wa sekta ya afya badala ya kuwapuuza.