- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE AITAKA SERIKALI KUWEKA MFUKO WA DAWA NA VIFAA TIBA
DODOMA: MBUNGE wa Viti Maalum,CECILIA PARESO ameishauri Serikali kuanzisha Mfuko maalum wa Dawa na Vifaa tiba katika sekta ya Afya kama ilivyo mifuko mingine ili kuwahahkikishia wananchi kupata dawa na vifaa tiba kwa uhakika.
Mheshimiwa PARESSO ametoa Kauli hiyo leo Bungeni mjini Dodoma wakati alipokuwa akiuliza swali la nyongeza.
Katika swali lake Mbunge huyo aliitaka serikali ifikirie kuwa Mfuko maalum wa Dawa na vifaa tiba katika sekta hiyo ya afya.
Pia amebainisha kuwa suala la upatikanaji wa vifaa tiba imekuwa ni tatizo hivyo kuitaka Serikali kusitisha uhamasishaji wa wananchi kujiunga na Mfuko huo wa CHF.
Akijibu swali hilo,Naibu Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) SELEMAN JAFFO amesema kuwa wazo la kuanzisha mfuko maalum wa dawa atalichukua kwani ni wazo zuri na watalifanyia kazi hivyo kuwataka wananchi kuendelea na huduma ya Mfuko wa CHF.
Hata hivyo MH.JAFFO amesema kuwa Mfuko wa huduma ya afya kwa jamii CHF umekuwa ukifanya vizuri katika baadhi ya maeneo nchini licha ya kuwepo kwa mapungufu katika baadhi ya maeneo.