- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE AITAKA SEREKALI KURUHUSU MATUMIZI YA BANGI NCHINI
Dodoma: Mbunge wa Kahama Mjini,Jumanne Kishimba kupitia CCM ameitaka Serikali ya Tanzania iruhusu matumizi ya bangi hapa nchini kwa kuruhusu wakulima walime mmea huo, huku akisema kwani dawa nyingi za maumivu zinatumia mmea huo.
Kauli hiyo ameitoa leo Mei 20 Bungeni wakati akichangia mjadala wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, kwa mwaka wa fedha 2018-2019.
Kishimba amesema dawa nyingi za maumivu zinatokana na bangi hivyo akaitaka Wizara ya Kilimo iwaruhusu wakulima ili walime.
“Sisi wenyewe tunayo bangi ukweli bangi hiyo sio kwa ajili ya kuvuta ni inaenda ,Lethoto na Zimbabwe wameruhusu.
“Gunia moja la bangi ni milioni 4 mpaka 5 bangi yote hii ya Tanzania inaenda katika madawa ya binadamu kuna ubaya gani Serikali itoe vibali ili watu walime bangi .Waziri wa Kilimo awasiliane na wa Afya kwani bangi hailiwi na wadudu ekari moja ya bangi unapata gunia sita,amesema Kishimba.
Akichombeza Spika Ndugai aliwataka Wabunge kuchangia kama ambavyo amechangia Mbunge huyo kwa kujikita katika eneo moja
“Niwape siri muongee kama Kishimba unakuja na kitu chako fulani.unajikita sehemu moja.
Hii hoja ni nzito sana Naamini Jenista (Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Ajira,Kazi,na watu wenye ulemavu) ameipigia mstari,”amesema Spika Ndugai.