- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBUNGE AITAKA SEREKALI KURUHUSU BANGI NCHINI SPIKA AMUUNGA MKONO
Dodoma. Mbunge wa Kahama Mjini (CCM), Jumanne Kishimba amemuomba Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, George Simbachawene kuwaruhusu wakulima wote wa bangi nchini kuiuza bangi yao katika kipindi cha miezi sita.
Mbunge huyo amesema kwa sasa wapo wakulima wa bangi wanaoshindwa kuiuza kwa kuwa kilimo hicho hakiruhusiwi nchini, na kutaka ambao wamelima zao hilo kupewa msamaha wa miezi sita ili waweze kuuza kabla soko la zao hilo kuporomoka.
Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Februari 3, 2020 bungeni mjini Dodoma katika mjadala wa kamati za Bunge.
Mara kadhaa mbunge huyo amekuwa akiitaka Serikali kuruhusu kilimo hicho kwa kuwa bangi ina soko kubwa ndani na nje ya Tanzania.
Akizungumzia kauli ya mbunge huyo, Spika Job Ndugai ameitaka Serikali kuangalia jambo hilo kwa mapana kwani nchi ya Canada inapata fedha nyingi kupitia zao hilo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama akisema Tanzania haina sheria ya kuruhusu kilimo cha bangi.