Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 4:53 pm

NEWS: MBUNGE ADAI WANANCHI WAKE WANAKABILIWA NA NJAA KALI

Dodoma. Mbunge wa Jimbo la Chemba mkoani Dodoma (CCM), Juma Nkamia amedai wananchi wa jimbo lake wamebaki na njaa kali baada ya kutakiwa na Serekali kumwaga vyakula kutokana na madai ya kuwa na sumu kavu na baada ya hapo wananchi hao kutelekezwa.

Tokeo la picha la juma nkamia

Nkamia ametoa kauli hiyo leo Jumanne Oktoba Mosi, 2019 katika uzinduzi wa mpango wa uwezeshaji wa kilimo cha matunda na mbogamboga Jimboni humo.

Hii si mara ya kwanza kwa mbunge huyo ambaye amewahi kuwa naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuibua madai hayo dhidi ya Serikali, amekuwa akieleza kuhusu wananchi wake kukabiliwa na njaa baada ya kutakiwa kumwaga vyakula vyao vinavyodaiwa kuwa na sumu kuvu. Ugonjwa wa sumukuvu umekuwa ukijirudia katika wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma kusababisha vifo vya watu katika maeneo hayo.

"Serikali ilikuja kuwalazimisha wananchi kumwaga chakula, watu walimwaga mahindi magunia mengi lakini leo wanalia njaa, Serikali haina mpango nao na kutuachia mimi na mbunge mwenzangu wa Kondoa (Dk Ashatu Kijaji- ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango), siyo jambo jema," amesema Nkamia.

Nkamia amesema gharama za mahindi zimefikia hadi Sh70,000 kwa gunia hivyo wananchi wengi hawawezi kuzimudu