- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBOWE: ''UPINZANI NI WITO''
ARUSHA:MWENYEKITI wa chama cha demokrasia na maendeleo [CHADEMA] Ambaye pia ni mbunge wa HAI FREEMAN MBOWE amesema kiongozi yoyote wa upinzani kunahitaji roho ngumu hata yeye kam a angekuwa ba moyo mwepesi na mpenda fedha angekuwa tayari ameshahama upinzani.
kauli hiyo ilitokana na diwani wa saba wa CHADEMA alipojiuzulu jana Mbowe alisema kiongozi wa upinzani awe mbunge, diwani, au mwenyekiti wa mtaa, kunahitaji roho ngumu na pia hiyo si kazi ya watu wenye kupenda fedha, bali ni ya maumivu, kudhalilishwa, kunyimwa ushirikiano, kufungwa wakati wowote na kunahitaji msimamo wa hali ya juu.
“Upinzani ni wito, wenye roho nyepesi hawawezi, kama ningekuwa napenda fedha, nina roho nyepesi, ningeshachukua hizo pesa na ningeshakimbia kabisa upinzani,” alisema.
Mbowe amesema hayo wakati chama hicho kikipitia misukosuko ya madiwani wake wa Mkoa wa Arusha kukihama na jana ilikuwa zamu ya Diwani wa Ambuleni, Arumeru, Japhet Jackson.
Diwani huyo aliwasilisha barua yake ya kuhama Chadema kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Meru, Christopher Kazeri jana mchana pia kama wenzake sita, akisema anamuunga mkono Rais John Magufuli.
Diwani wa karibuni kujiuzulu wa Ngobobo, Solomon Laizer pia wa wilaya hiyohiyo katika jimbo linaloongozwa na Joshua Nassari wa Chadema.