- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBOWE NA WENZIE WASAMEHEWA.
Dodoma: Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania limetoamsamaha kwa mkuu wa wilaya ya Arumeru Mnyeti, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na kiongozi rasmi wa upinzani bungeni Freeman Mbowe bila masharti yoyote kutokana na makosa mbalimbali waliyoyafanya.
Pia limemsamehe mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya na kupewa barua ya onyo na Mbunge wa Kawe Halima Mdee kwa sharti kwamba akifanya kosa lingine lolote atapata adhabu ya kupelekwa kwenye kamati ya maadili na madaraka ya Bunge
Akiwasilisha taarifa ya kamati leo Bungeni mjini Dodoma makamu mwenyekiti wa Almas Maige amesema Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na Mnyeti waliitwa na kamati kwa kosa la kudharau, kuvunja haki na kuingia uhuru wa bunge kosa ambalo walikiri kutenda na kuomba msamaha mbele ya kamati.
Amesema imeelezwa kuwa Mdee na Mbowe kwa nyakati tofauti walidharau mamlaka ya spika ambapo baada ya kuitwa na kamati husika walikiri na kuomba msamaha
Naye waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu sera, bunge.kazi,vijana, ajirana watu wenye ulemavu Jenista Mhangama ametoa tahadhari kwa wabunge hao kuheshimu msamaha uliotolewa.
Spika wa Bunge Job Ndugai amewata Wabunge kuheshimiana lakini vikao vya kamati vitumike kuwafundisha wabunge maadili.