Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 1:22 am

NEWS: MBOWE NA MATIKO WASHINDA RUFAA YAO DHIDI YA SEREKALI

Dar es Salaam: Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Mh. Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko kwa pamoja wameshinda rufaa ya dhamana yao dhidi Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) katika Mahakama ya Rufani jijini Dar es salaam.

Leo Machi 1, 2019 Mahakama imetoa uamuzi huo baada ya DPP kukata rufaa Mahakama ya Rufani akipinga uamuzi wa Mahakama Kuu wa kukubali kuendelea na usikilizwaji wa rufaa ya wabunge hao ya kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwafutia dhamana.

DPP aliweka pingamizi la awali akiiomba Mahakama hiyo isiisikilize rufaa hiyo pamoja na mambo mengine akidai haina mamlaka kwa kuwa ilikuwa inakiuka matakwa ya sheria. Jaji Sama Rumanyika alitupilia mbali pingamizi hilo DPP badala yake akaamua kuendelea na usikilizwaji wa rufaa hiyo ya kina Mbowe, lakini kabla ya kuanza kuisikiliza DPP akakimbilia Mahakama ya Rufani kukata rufaa kupinga uamuzi huo.

Mbowe na Matiko walifutiwa dhamana na aliyekuwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri Novemba 23 mwaka huu baada ya kushindwa kufika mahakamani kwa ajili ya kesi ya jinai inayowakabili mahakamani hapo pamoja na viongozi wengine saba wa chama hicho.

Kufuatia uamuzi huo, Mbowe ambaye ni mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro na Matiko mbunge wa Tarime Mjini, walikata rufaa Mahakama Kuu siku hiyohiyo wakipinga kufutiwa dhamana yao chini ya hati ya dharura sana.

DPP aliiomba Mahakama hiyo itengue uamuzi wa Mahakama Kuu wakidai ilikosea kukubali kusikiliza rufaa hiyo ya kina Mbowe kwa kuwa ilikuwa inakiuka matakwa ya kisheria