Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 3:38 am

NEWS: MBOWE NA MATICO WARUDISHWA SEGEREA, KESI YAO YAHAIRISHWA

Kesi Na.112/2018 inayowakabili Viongozi wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Freman Mbowe na Wabunge 7 wa Chama hicho, imehairishwa hadi Alihamisi ya Febuari 28, mwaka huu.

Na wakati huo huo Tarehe 18 mwezi Februari Mwaka huu Mahakama ya Rufaa itasikiliza rufaa ya serikali kutokana maamuzi madogo ya Mahakama Kuu juu ya dhamana ya M/kiti Freeman Mbowe na Ester Matiko

Novemba 23, 2018 Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini Esther Matico kwa pamoja walifutiwa dhamana na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu baada ya Viongozi hao kukiuka masharti ya dhamana zao.

Sababu zilizotolewa ni kwamba Mbowe alishindwa kuhudhuria mahakamani tarehe 8 November 2018 baada ya kuugua ghafla na kwenda Afrika kusini kwa matibabu.

Mwezi Oktoba 28,alielekea Washing DC Marekani kuhudhuria mkutano na aliporejea tarehe 31 Oktoba aliugua ghafla.

Wakati huohuo mbunge wa Tarime mjini, Esther Matiko pia alifutiwa dhamana wa kukiuka masharti.

Matiku alishindwa kuhudhuria mahakamani baada ya kwenda kwenye ziara ya wabunge nchini Burundi, sababu ambayo alielezwa kwamba haikidhi matakwa ya kushindwa kufika mahakamani.

Washtakiwa wote wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwamo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari mosi na 16, mwaka 2018 maeneo ya Dar es Salaam.