- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBOWE AWATAKA WASIOTAKA KUJITOLEA CHADEMA WASEPE
Dar es salaam: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe amesema mwanachama yeyote wa chama hicho ambaye ameona wajibu wa kujitolea ameuwona mzito ni bora asiwepo kwenye chama hicho, "unapoona watu wanafungwa hujatolea tamko, unapoona mtu anapigwa risasi usione uovu ni bora ukishindwa kulia na sisi usiwe na sisi" amesema Mbowe
Mbowe ametoa kauli hiyo Leo Ijumaa Machi 15, 2019 wakati akiongea na Waandishi wa HABARI jijini Dar es salaam
Mbowe amezungumzia pia swala la Spika wa bunge Job Ndugai kufuta posho na stahiki za kibunge za mbunge wa singida mashariki Tundu Lissu, Mbunge huyo wa HAI amewataka viongozi wenye mamlaka waone aibu juu swala hili na kusema kuwa ikiwa hao wenye mamlaka Lissu angekuwa ni mwanao kapigwa Risasi na kaponeshwa kimiujiza walitaka Lissu alie
"Kuhusu mbunge Tundu Lissu mshahara wake inasemekana umezuiliwa sisi kama chama tunasema hebu tupate aibu kidogo tuvae ubinadamu, hao wenye mamlaka wafikirie Lissu angekuwa mtoto wao amepigwa risasi akapona kimuujiza huyu mtu mlitaka aliye" amesema Mbowe
Mbowe na Matiko walikuwa Gerezani Segerea baada ya kufutiwa dhamana na hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi kisutu kwa kile kilichotajwa kuwa ni kukiuka masharti ya dhamana na baadae wakakata rufaa katika mahakama kuu dhidi ya kufutiwa dhamana hiyo.
Machi 7, 2019 mahakama kuu ya Tanzania ikawaachia huru wabunge hao .