Home | Terms & Conditions | Help

November 27, 2024, 9:30 am

NEWS: MBOWE APOKONYWA OFISI YA UBUNGE AKIWA MAHABUSU

Arusha: Mkuu wa wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amemnyang'anya ofisi ya Ubunge, Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe baada ya kueleza hajaitumia tangu mwaka 2010.

Ofisi hiyo ilikwa ya Mbunge kwa zaidi ya miaka 20 sasa itakuwa inatumiwa na idara ya uhamiaji wa halimashauri hiyo.

Alipoulizwa leo Januari 14, 2019 mkuu wa wilaya huyo Sabaya amesema lengo la Serikali kutoa ofisi kwa mbunge huyo ilikuwa ni kusaidia wananchi lakini ofisi hiyo imekuwa haifunguliwi. "Tangu mimi nimeteuliwa kuwa Mkuu wa wilaya hapa mwezi wa nane (mwaka jana) ofisi haijafunguliwa sasa kwa kuwa kuna uhitaji wa ofisi muhimu ya uhamiaji nimeamua kuwapa," amesema.Tokeo la picha la Lengai Ole Sabaya na mbowe

Ofisi hiyo inapatikana katika jengo la mkuu wa wilaya hiyo, ambapo pia zipo ofisi za halmashauri ya wilaya ya Hai.

Amesema amepata taarifa pia tangu Mbowe achaguliwe mwaka 2010 hajawahi kuingia tena katika ofisi hiyo kusikiliza kero za wananchi. "Sijui yupo wapi ila namsikia huko maeneo mengine akifanya vurugu sasa ofisi hii itatumika kusaidia wananchi," amesema.

Mbowe ambaye ni mwenyekiti wa Chadema amekuwa mbunge wa Hai kwa awamu ya tatu na ofisi hiyo imekuwa ya mbunge na kuwekewa kibao cha ofisi ya mbunge kwa zaidi ya miaka 20.