- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBOWE AMUANDIKIA BARUA RAIS MAGUFULI KUOMBA MARIDHIANO
Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema kuwa kimemuandikia Barua Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli kuomba maridhiano ya amani baina ya Serekali, vyama vya Siasa na Mashirika yasiyo ya kiserekali ili kuepusha taifa kuingia katika machafuko hapo baadae hasa wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao.
Akiongea na Waandishi wa Habari leo Febuari 3, 2020 Mwenyekiti wa Chadema Taifa Freeman Mbowe amesema kunatatizo kubwa la Demokrasia katika nchi ya Tanzania licha ya viongozi waliomamlakani kutojali.
"Rais achukue hatua asije baadaye akatulaumu, wapo wadau wengi, napozungumza maridhiano simaanishi viongozi wa vyama vya siasa pekee tukae tuzungumze kuna mambo hayapo sawa dunia inatushangaa," Freeman Mbowe,
"Hatutamani wala hatuombei taifa hili kuingia kwenye machafuko, lakini mwaka wa uchaguzi ndio mwaka unaozaa machafuko, kuna tatizo kubwa la demokrasia katika nchi hii lakini watawala wetu wamejaa kiburi," Freeman Mbowe, M/Kiti Chadema.
Mbowe amabye ni Mbunge wa Hai amesema kuwa Kubezwa ama kupuuzwa kwa viongozi wa upinzani na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni utamaduni uliojengeka kwa muda mrefu lakini busara zinawatuma "kutotumia ujinga wa wenzetu kuliingiza taifa kwenye machafuko,"
"Kila jambo lina majira yake hivyo tunalazimika kuweka kumbukumbu sahihi, tumetoa matamko, wameandika waandishi wa habari lakini watawala wamekaa kimyaa kana kwamba hawasikii, hatuwezi kuacha kutoka kuipigania haki wakati huo tukiitafuta amani," Freeman Mbowe, M/Kiti Chadema.
Desemba 9, 2019 Mbowe katika ujumbe wake kwa taifa wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika (Tanzania Bara) alieleza ulazima wa kuwepo maridhiano, upendo na mshikamano katika taifa la Tanzania.
”Rais una nafasi ya kipekee kuweka historia ya maridhiano katika taifa letu kwani kuna wengine wanalalamika wanaumia. Rais tumia nafasi hii ukaliweke taifa katika hali ya utengamano,” amesema Mbowe.
“Nimekuja kushiriki sherehe za miaka 58 ya Uhuru kama uthibitisho wa ulazima wa kuwepo maridhiano, upendo, mshikamano katika taifa letu. Namuomba Mungu siku ya leo ikafungue milango tuweze kuishi kama taifa linalopendana, tuvumiliane, tukosoane, turuhusu demokrasia
Mbowe alishiriki katika maadhimisho hayo huku akiwa na kesi ya uchochezi mahakamani kwa zaidi ya mwaka sasa, sambamba na viongozi wenzake nane, lakini pia kukiwa na zuio la kutofanya mikutano ya hadhara.
Pia, kumekuwa na malalamiko ya vyama vya upinzani kuhusu kubinywa kwa demokrasia nchini, hivyo ujumbe wa Mbowe unamuomba Rais Magufuli kujenga maridhiano kati ya serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wapinzani.
Mbali na Mbowe, viongozi wengine wa Chadema waliohudhuria sherehe hizo ni Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Kati, Lazaro Nyalandu; Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Bara na Mbunge wa Kibamba, John Mnyika; na Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema; Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche na wengine.