- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBOWE AKAMATWA KWA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI HAI
Jeshi la Polisi wilayani Hai linamshikilia Mwenyekiti wa Chama cha upinzani Chadema na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe akiwa katika mkutano wa hadhara na wananchi wake. Polisi wamemkamata muda mfupi baada ya kumaliza mkutano wa hadhara katika viwanja vya Nkoromu. Polisi wamemuhoji juu ya kwanini amezungumzia swala la Tume huru Jimboni kwake. Wakili John Malya,amedhibitisha tukio hilo.
Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni alikamatwa saa 12:00 baada ya kumaliza mkutano uliohudhuriwa na mamia ya wananchi. Wakati akijiandaa kuondoka eneo hilo, polisi walikwenda katika gari lake wakieleza kuwa wanamhitaji kituoni, ombi ambalo liliridhiwa na mwenyekiti huyo wa Chadema.
Awali, akizungumza katika mkutano huo Mbowe amesema licha ya kupitia kipindi kigumu na changamoto mbalimbali za kisiasa, hawezi kukoma kuendelea na mapambano.
Huku akisisitiza kuwa hajawahi kupitia kipindi kigumu katika siasa kama sasa, Mbowe amesema, “kufa sijafa lakini cha mtemakuni nimekiona, nimekaa jela, mahabusu na mahakamani nimekwenda lakini sikomi ng'o, ndio kwanza wananitia moto.” Amesema haogopi haogopi kufa wala kwenda jela, huku akigusia umuhimu wa kujenga miundombinu ya barabara na reli na kuwaacha wananchi kuwa huru.
"Hakuna kitu chenye thamani katika maisha yenu kama uhuru wenu, mkijengewa barabara, shule lakini mkanyimwa uhuru wenu ni bora mvikose hivyo vyote lakini mpate uhuru wenu na hayo ndiyo maneno ambayo Chadema tumehubiri,” amesema Mbowe.