- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBOWE AIBANA SERIKALI ITEMBELEE HOSPITALI YA HAI
MBUNGE wa Hai na Kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe (Chadema)leo bungeni ameibana serikali na kutaka ieleze ina mkakati gani wa kuinusuru hospitali ya wilaya ya Hai mkoani kilimanjaro.
“Hospitali ya Hai ilianza kujengwa kwa miaka kumi liyopita wakati huo mji ukiwa na watu wasiozidi 10,000 na mji wa Hai ni mji unaokuwa kwa kasi na kwa sasa mji huo kwa sasa una wakazi wanaozidi milioni 50.
“Hospiatal hii imekuwa ikijengwa kwa awamu awamu lakini kwa sasa kuna tatizo kubwa na la msingi kwa sasa wanaume na wanawake wanalala katika wodi moja na mitembelea hospitahi hii kwa wiki moja iliyopita na nimeshuhudia hali hii.
“Ninachomuomba Naimbu waziri kwa sasa kutokana na unyeti wa hospitali hii na ikiwa pia hospitali hii kuwa katika barabara kuu ya Arusha- Moshi na ukizingatia watu wengi wanapata ajali wanapelekwa katika hospitali hiyo.
“Je Naibu Waziri huko tayari kutenga muda wako kwa ajili ya kitembelea hospitali ile tuone kwa pamoja tatizo lililopo kisha serikali itafute ufumbuzi wa kutatua tatizo hilo”. Amehoji Mbowe
Awali katika swali la msingi la mbunge wa Viti Maalum,Juliana Shonza (CCM) ametaka kujua ni lini serikali itajenga wodi ya akina mama ambayo ni kubwa yenye vifaa vya kutosha katika wilaya ya Mbozi na Momba ili wanawake waondokane na adha ya kulala wawili wawili.
Akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbowe, Naibu Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais –TAMISEMI Selemani Jafo ,amesema kwa takribani kwa wiki tisa au kumi alikuwepo katika hospitali hiyo pamoja na kuona juhudi zinazofanywa katika kuhakikisha hospitali hiyo inajengwa kwa kuzingatia mahitaji.
Amesema katika ziara hiyo alifarijika kuona ujenzi wa wodi ya akina mama unaoendelea,pia alikiri kuwepo kwa matatizo mbalimbali huku akieleza kuwa yupo tayari kufika na muuliza swali kwa lengo la kuona ni jinsigani ya kuboresha ujenzi wa wodi ya akina mama.
Akijibu swali la msingi Jaffo amesema Hospitali ya wilaya ya Mbozi(Vwawa) ni hospitali iliyoiliyopandishwa adhi kutoka kituo cha afya kuanzia mwaka 2001.
Amesema kwa sasa hospitali hiyo inawahudumia wagonjwa wengi kutoka halmashauri ya mji wa Tunduma,wilaya Maomba,wilaya ya mbozi na Wilaya ya Ileje.