- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBOWE AHOJI KUKIUKWA KWA KANUNI ZA UCHANGUZI SEREKALI ZA MITAA
Dodoma. Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema , Freeman Mbowe amehoji leo Bungeni kuwa je ni sahihi kwa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2019 kuanza kutumika kabla ya Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo kuziona.
Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni nchini Tanzania amesema inawezekana watu wakaona mambo (uchaguzi) hayo ni mepesi lakini amani ya nchi itapotea ama kuathirika kama yasipowekwa sawa.
Mbowe amehoji leo Alhamisi Septemba 5 2019, wakati alipopata nafasi ya kuuliza swali la nyongeza katika kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma.
Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai amesema sheria ndogo na kanuni zinazotungwa zozote nchini ni lazima ziangaliwe Bungeni lakini vikao vinavyokaa kujadili mabadiliko ya sheria haviwezi kuwa mbadala ya Bunge.
Amesema kamati ya Sheria Ndogo haijawahi kuona wala kupitia kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“Mheshimiwa Waziri atueleze katika utamaduni huo ambako tayari kanuni zimeshaingizwa kazini kamati ya Sheria Ndogo haikuzipitia kwa kisingizio wadau walipitia ni jambo hili ni sahihi,” amehoji Mwenyekiti huyo wa Chadema
Akijibu swali hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania (AG), Profesa Adelardus Kilangi amesema sheria ndogo zikishatayarishwa huwa zinapelekwa katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa uchambuzi.
Amesema baada ya uchambuzi, hurudishwa kwa waziri mhusika ambaye huchapisha katika Gazeti la Serikali halafu baada ya hapo hupelekwa katika kikao kinachofuata cha Bunge kwenye kamati ndogo ya sheria kwa ajili ya kuchambuliwa.
Amesema kimsingi sheria ndogo inatungwa chini ya sheria mama na kuna misingi inayofuatwa na kwamba mojawapo ya misingi hiyo ni isipingane na sheria mama. Amesema baada ya kupelekwa bungeni kama kuna changamoto, kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo hutoa maelekezo na Serikali hurekebisha. “Mheshimiwa mwenyekiti hakuna tatizo lolote katika eneo lolote,” amesema.
Katika maswali ya nyongeza, Mbunge wa Kibamba (Chadema), John Mnyika amesema Katiba inasema Bunge linaweza kutunga sheria ya kuipa jukumu lolote Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).
Amesema pamoja na hilo, Nec haikuwa na jukumu la kusimamia kura ya maoni lakini Bunge lilitunga sheria ya kusimamia kura ya maoni. “Kwanini Serikali imeogopa kuleta bungeni sheria ya kuipa mamlaka ya kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa. Hiyo ingeondoa waziri kusimamia uchaguzi,” amehoji.