- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBATIA KWENDA MAHAKAMANI KUMZUIA NDUGAI KUJIUZULU
Dar es salaam. Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia amesema kuwa anakusudia kwenda kufungua kesi mahakamani ya kupinga mchakato alioutumia Spika wa Bunge Job Ndugai kujiuzulu hapo Jana.
Mbatia ameeleza kuwa mpaka sasa bado anamtambua Job Ndugai kama Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania.
"Utaratibu uliofanyika jana wa Job Ndugai kujiuzulu Uspika wake, kwa mujibu wa katiba ya Tanzania ibara ya 149 haikufuatwa, kwa hiyo ndugu Ndugai mpaka sasa hivi bado ni Spika, alitakiwa kwenda kujiuzulu mbele ya kikao chake cha bunge" amesema James Mbatia.
Jana Januari 6, 2022 Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai alitangaza kujiuzulu wadhifa wake.
Kwa mujibu wa barua ya Spika Ndugai aliyomuandikia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema uamuzi huo wa kuachia nafasi hiyo ameufanya kwa hiari.
"Naomba kutoa taarifa kwa umma wa Watanzania kuwa leo Tarehe 06 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa bunge la Jamhuri .." imesema sehemu ya taarifa hiyo nakuongeza;
"Pia nakala yangu hiyo ya kujiuzulu nimewasilisha kwa katibu wa Bunge kwa ajili ya hatua stahiki kwa mujibu wa katiba ya nchi na sheria nyingine" amesema Ndugai kwenye taarifa yake kwa umma.
Ndugai ambaye ni mbunge wa Kongwa amesema anawashukuru wabunge, Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali, wananchi wa Jimbo la Kongwa na Watanzania wote kwa ushirikiano waliompa kipindi akiwa Spika