- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBARONI KWA KUMBAKA MWANAMKE AKIJIFUNGUA
Katavi. Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linamshikilia muuguzi msaidizi wa kituo cha afya Mamba Wilaya ya Mlele, Mkoani Katavi Abednego Nkona (32) kwa tuhuma za kumbaka mjamzito wakati akitaka akijifungua.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dec 19, 2019 Kamanda wa Polisi mkoani Katavi, Benjamin Kuzaga alisema tukio hilo limetokea juzi saa 2.00 usiku.
Alisema mjamzito huyo alifika katika kituo hicho cha afya kwa ajili ya kujifungua na wakati mtuhumiwa akimpima njia, alimbaka.
“Mwanamke huyo alihisi hali isiyokuwa ya kawaida sehemu zake za siri, alishtuka na kumuona mtuhumiwa amemuingilia kimwili.
“Baada ya kufanyiwa kitendo hicho, mjamzito alinyanyuka kitandani na kwenda kutoa taarifa kwa mzazi mwenzake wake Mektrida Deogratius mkazi wa Majimoto,” alisema.
Polisi mkoani Katavi wanatarajia kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo wakati wowote ili kujibu tuhuma zinazomkabili.