- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MBARONI KWA KUANZISHA MTANDAO WA CORONA TANZANIA
Jeshi la Polisi mkoani Morogoro linanshikilia kijana anayeitwa Awadhi Luguya (24), mkazi wa Mazimbu, Manispaa ya Morogoro kwa tuhuma za kufungua ukurasa wa 'Fecebook' wenye jina 'Coronavirus Tanzania.
Jeshi la polisi limetoa taarifa hiyo jana Aprili 4, 2020 likidai kuwa kijana huyo alikuwa akichapisha taarifa zisizo rasmi kwenye ukurasa huo kuhusu mlipuko wa virusi vya Corona nchini zinazolenga kupotosha wananchi na hazina ukweli wowote.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa amesema mtuhumiwa alikamatwa Aprili 1, mwaka huu, majira ya saa 11 jioni katika eneo la Mazimbu.
Amesema polisi walipata taarifa kutoka kwa wananchi na kupitia mitandao ya kijamii kuwa kijana huyo amefungua ukurasa huo na anautumia kutoa taarifa ambazo sio rasmi, na zilizojaa upotoshaji mkubwa kwa watu kuhusu Corona.
“Tumemkamata na simu zake zote. Anaendelea kuhojiwa na atafikishwa mahakamani kwa makosa ya matumizi mabaya ya mtandao,” amesema Mutafungwa.
Kwa mujibu wa Wizara ya Afya nchini Tanzania Jumatano Aprili 1 ilitangaza ongezeko la mgonjwa mmoja wa virusi vya corona nchini humo hali inayofikisha idadi ya wagonjwa nchini humo kufikia 20.
Taarifa ya Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, mgonjwa huyo ni mwanamke mwenye miaka 42 na raia wa Marekani.
Taarifa ya Bi Mwalimu inaeleza kuwa mgonjwa huyo mpya alikuwa karibu na mtu aliyesafiri nje ya nchi na baadaye kuthibitika kuwa ana maambukizi ya virusi hivyo baada ya kurejea Tanzania.
Katika taarifa hiyo bi Ummy pia amethibitisha kuwa tayari wagonjwa wawili nchini humo wamepona virusi hivyo.
Tarehe 31 Machi, mwaka huu mmoja kati ya wagonjwa waliokuwa katika kituo cha matibabu cha Temeke Dar es Salaam amethibitika kupona maambukizi aliyokuwa nayo na ameruhusiwa kurudi nyumbani na hivyo sasa kufanya jumla ya watu waliopona kuwa watatu," imeeleza taarifa ya waziri Ummy.
Jumanne ya Machi 31, 2020 Tanzania ilitangaza kifo cha kwanza cha mgonjwa wa virusi vya corona nchini humo.
Mpaka sasa kwa mujibu wa waziri kuna wagonjwa 17 ambao bado wanaendelea na matibabu na hali zao zipo vizuri.
Jumatatu wiki hii waziri Ummy alibainisha kuwa serikali imekuwa ikufatilia "watu wote wa karibu waliokutana na wagonjwa (contact tracing)," na kuwataka wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhai ili kujikinga na ugonjwa huu," ameeleza Bi Mwalimu.
Siku hiyo alitangaza wagonjwa watato, watatu kutoka Dar es Salaam na wawili kutoka Zanzibar.