- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAZOEZI YA VITENDO YA SHEREHE ZA MUUNGANO YAWAVUTIA WAKAZI WA DODOMA
Dodoma: Ikiwa imebaki siku moja ili serikali ifanye maadhimisho ya miaka 53 ya sherehe za Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ,leo yamefanika mazoezi kwa vitendo kwa ajili ya kuboresha ufanisi wa sherehe hizo ambazo zitafanyika katika viwanja vya Jamhuri mjini hapa.
Maadhimisho hayo yatafanyika kwa mara ya kwanza katika mkoa wa Dodoma, kutokana na adhi ya mkoa wa Dodoma kuwa makao makuu ya nchi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana,ameeleza kuwa sherehe hizo zitakuwa zikifanyika mkoani hapa kila mwaka ili kujenga adhi ya Dodoma kuwa makao makuu.
Viongozi mabalimbali wa kitaifa na kimataia wanatarajiwa kuudhuria sherehe hizo huku wake wa waasisi wa Muungano wakitarajiwa kupamba sherehe hizo pamoja marais wastaafu pamoja na mawaziri wote wastaafu, samamba na wageni wengine waarikwa kutoka nchi za nje.
Wananchi waetakiwa kuhudhuria ili kuweza kujionea vikundi mabalimbali vya michezo kikiwemo kikundi cha makomandii,urushaji wa ndege za kivita pamoja na michezo mbalimbali na vikundi vya burudani.