Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 4:33 pm

NEWS: MAVUNDE AZINDUA MFUMO MAALUMU WA VIPIMO VYA AFYA

DODOMA: MBUNGE wa jimbo la Dodoma Mjini na NAIBU Waziri wa Ajira,Kazi,Vijana na Walemavu Mh.Antony Mavunde leo amezindua mfumo maalumu wa vipimo vya kibaiolojia (Biometric Systerm) na CCTV Camera katika Hospital ya Rufaa ya Dodoma utakaosaidia kuboresha huduma za Afya na kupunguza kero za wananchi.


Akizungumza na wananchi waliofika hospitalini hapo kwa ajili ya kupatiwa huduma,mara baada ya ukakuzi wa vifaa hivyo Mh.Mavunde amesema mfumo huo utasaidia kwa kiasi kikubwa wananchi kupata huduma bora sambamba na kutambua uwajibikaji wa wafanyakazi


Sambamba na kumpongeza Mh,Mvunde kwa hatua hiyo Mganga Mfawidhi wa Hospital hiyo Dr.Caroline Damian amesema tangu kufungwa kwa mfumo huo ufanisi wa kazi umeongezeka na malalamiko yamepungua kwa kiasi kikubwa na kuwa bado kuna uhitaji mkubwa wa vifaa hivyo


Donatus Bashemerwa ni Afisa Muuguzi katika hospital ya Rufaa ya Dodoma yeye amesema hatua ya kufunga mifumo hiyo ni mzuri kwani pia utawasaidia wao kama watumishi kupata stahiki zao pindi wanapofanya kazi kwa muda wa ziada


Hatua ya Mh,Mavunde kufunga mifumo hiyo katika hospital ya Rufaa ni muendelezo wa utekelezaji wa ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni kwa wanachi wa Jimbo la Dodoma Mjini ambapo hata hivyo ameahidi kuendelea kuwaboreshea huduma mbalimbali