- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAVUNDA AWATAKA VIJANA KUJITOA KIVITENDO NA SIO MANENO
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Vijana Anthony Mavunde amewataka vijana kuwa wazalendo kwa vitendo kwa kujitoa na nchi yao na sio kwa maneno.
Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo wakati akikabidhi bendera kwa vijana NANE wanaopanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukizi ya miaka 20 ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Amesema vijana wengi wanakosa uzalendo kutokana na kushindwa kuitetea nchi yao kwa vitendo badala yake wamekuwa wakiongea kwa maneno tu bila kuwa na vitendo.
Amesema uzalendo hauishii kwenye kutamka tu mdomomi bali ni matendo yanayoendana sambamba na maneno yenyewe na kubeba uzito.
Nae Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana ofisi ya Waziri Mkuu, James Kajugusi amesema vijana hao ni kundi la pili la vijana 100 ambao wanatakiwa kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukizi ya Baba wa Taifa Hayati Julius Kambarage Nyerere kabla ya kilele chake kitakachofanyika mkoani Lindi October 14 mwaka huu.