Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 1:51 pm

NEWS: MATUMIZI YA SHISHA YATAKIWA KUPIGWA MARUFUKU

DODOMA: Mbunge wa Viti Maalum Najma Murtaza Giga (CCM) ,ameitaka Serikali kupiga marufuku matumizi ya Shisha ambapo amedai imekuwa ikiwaathiri Vijana wengi.

Akiuliza swali bungeni Giga amesema,watumiaji wa Shisha wamekuwa wakichanganya na aina mbalimbali za dawa za kulevya na vileo vikali na kusababisha Vijana wadogo kuathiriwa kwa kiasi kikubwa.

"Je kwa nini Serikali hadi sasa inaendelea kuruhusu matumizi ya shisha kwenye baadhi ya migahawa na hoteli kubwa ambayo inatumiwa na watu wa rika zote.?" alihoji Giga
Akijibu swali hilo,Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amesema,Serikali inao mpango wa mkakati wa kutengeneza utaratibu wa kulidhibiti na kuitungia sheria ili kupiga marufuku utumiaji,uuzaji na usafirishaji wa shisha nchini.

kushoto ndiye Najma Murtaza Giga (CCM)

Amesema lengo la kufanya hivyo ni kuokoa Afya za watanzania walio wengi ambao ni nguvu kazi kwa Taifa la Tanzania.

."Hata hivyo tukiwa tunasubiri kutungwa kwa Sheria na kanuni,Mheshimiwa Waziri Mkuu aliunga na na Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Dar es Salaam kupiga marufuku matumizi ya Shisha mnamo Julai mwaka 2016. Alisema Nchemba

Katika swali la nyongeza Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) alitaka kujua namna Serikali inavyowasaidia Vijana wanaotumia Shisha pamoja na dawa za kulevya kwa ujumla kwa kuwa watumiaji wengi we dawa za kulevya ni wake waliokata tamaa ya maisha.


Akijibu swali hilo Waziri wa Afya ,Mendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema,ili kuwanusuru vijana hao walikata tamaa na kujiingiza katika matumiziya dawa za kulevya,Serikali inaendelea kutoa elimu kupitia runinga ,radio na vijarida mbalimbali.

Amesema,wale waliokuwa wanatumia dawa za kulevya wameanza kupewa dawa kama tiba ya kuachana na dawa hizo lakini pia ametoa wito kwa jamii kushirikiana na Serikali katika kuwaelimisha vijana ili waweze kuacha dawa hizo kwa kuwa vita hiyo siyo ya Serikali pekee yake.