Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:26 pm

NEWS: MATAIFA YA G7 KUICHUNGUZA AFRICA NA KOREA KASKAZINI

Sicily: Viongozi wa nchi zilizostawi kiuchumi Duniani Maarufu kama G7 wanataraji kukutana na viongozi wa bara la Afrika baadae kwa mazungumzo juu ya janga la wahamiaj, Viongozi hao wanakutana na viongozi wa mataifa ya Afrika Jumamosi(27.05.2017)siku ya mwisho ya mkutano wao wa kila mwaka ambao umegubikwa na kutokukubaliana kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.

Mkutano huo unaofanyika Sicily nchini Italia ambapo inchi kama Uigereza, Ujerumani, Japan, marekani ufaransa na kanada zimeendelea kufanya mazungumzo.

Viongozi kutoka Tunisia, Kenya, Ethiopia, Niger na Nigeria watazungumza na wakuu hao katika siku ya pili ya mkutano wa G7 mjini Taormina, Sicily.

Italia ilichagua kuwa mwenyeji wa mkutano huo ili kuvutia umakini kwa Afrika na mamilioni ya wahamiaji ambao wamekuwa wakihatarisha maisha yao kuelekea Ulaya.


Hata hivyo mjadala mkali ambao umeendelea kutawala vikao vya G7 ni kuhusu ugaidi na mabadiliko ya tabia nchi. Pia viongozi wa G7 wamesema kuna makubaliano makubwa kuhusiana na masuala kadhaa yanayobishaniwa ya sera za mambo ya kigeni , ikiwa ni pamoja na Syria , Libya na Korea kaskazini.