Home | Terms & Conditions | Help

November 24, 2024, 7:51 pm

NEWS: MATAIFA YA AFRIKA YAALANI MPANGO WA TRUMP MASHARIKI YA KATI

Viongozi wa Afrika wameulaani vikali mpango wa amani ya Mashariki ya Kati uliopendekezwa na Rais Donald Trump wa Marekani wanaosema si halali.

Viongozi wa mataifa ya Afrika ambao wamekuwa wakikutana jijini Addis Ababa nchini Ethiopia, wamesema mpango huo haukubali na unaipendelea Israel na kuionea Mamlaka ya Palestina na hivyo unakwenda kinyume na maamizio ya Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kuhusu namna ya kutatua mzozo kayi ya Israel na Palestina.

Rais wa Misri anayemaliza muda wake kama Mwenyekiti wa Umoja huo Abdel Fattah al-Sisi, amesema kuwa Palestina itaendelea kuwa mioyoni mwa waafrika, huku Mwneyekiti mpya rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa, akisema mapendekezo ya Marekani ni kitendo cha ubaguzi kama ilivyokuwa nchini Afrka Kusini wakati wa kipindi cha ubaguzi wa rangi.

Viongozi hao wa Afrika pia wamekuwa wakizungumzia kuhusu mizozo mbalimali katika mataifa hayo. Suala la tishio la ugaidi hasa katika mataifa ya Sahel, nchini Somalia na mzozo wa Sudan Kusini ni miongoni mwa changamoto ambazo viongozi hao wanajaribu kuzitafutia ufumbuzi bila kusahau ukosefu wa usalama nchini Libya.

Mkuu wa Tume ya Umoja wa Afrika Moussa Faki Mahamat amesema hatua zaidi zinastahili kuchukuliwa ili kutatua changamoto hizo, ambazo amesema zinaanza kwa kutatua hali ya umasikini inayowakumba waafrika wengi.