- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MASHINJI AMTAHADHARISHA MKUU WA MAJESHI KUINGIZWA KWENYE SIASA
Dar es salaam: Katibu mkuu wa chama Cha Demokrasia na Maendeleo chadema Dkt Vicent Mashinji amemtaka mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama nchini Jenerali Venance Mabeyo Kutokubali kuingizwa kwenye mkenge wa kisiasa hapa nchini.''Wasikuingize kwenye siasa kamanda wetu. Kazi yako inahitaji sana akiba ya maneno" amesema Dkt Mashinji.
Kupitia ukurasa wake wa twitter Dkt Mashiji alimuandikia Ujumbe Jenerali Mabeyo leo jumamosi kumsihi kamwe asikubali hata kidogo kuingizwa kwenye siasa, kwani yeye kama mkuu wa majeshi ndio mwenye dhamana ya kurekebisha pale ambapo nchini itakapokuwa na matatizo. " Ikitokea umevuruga hakuna tena wa kurekebisha. Ndo maana “Generals speak by Actions!”
Kauli ya Dkt Mashinji imekuja mara baada ya Mkuu huyo wa Masheji leo kusema kuwa wao kama jeshi wanaendelea kufuatilia kauli tata zinazoashiria uchochezi na kuhatarisha kuibua machafuko ndani ya nchi, na kuongezea kuwa jeshi hilo pia lipo tayari kukabiliana na machafuko ambayo yanaweza kujitokeza kutokana na uchochezi huo.
"Ndani ya nchi yetu kwa kushirikiana na vyombo vingine tutawalinda wananchi na mali zao, tutakabiliana na matishio ndani ya nchi yetu, na sasa hivi tunaendelea kufuatilia kauli tata zinazoashiria uchochezi na machafuko ndani ya nchi yetu" amesema Jenerali Mabeyo
Kauli hiyo ya Jenerali Mabeyo ameitoa leo Jumamosi April 13, 2019 wakati wa hafla ya uzinduzi wa mji wa kiserikali uliojengwa Ihumwa mkoani Dodoman ambao unakusudiwa kunaziduliwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli.
Mabeyo amesema kwasasa hali ya nchi ni shwari ila jeshi linaendelea kuimarisha ulinzi wa wananchi na mali zao kuhakikisha amani inaendelea kutawala. “Hali ya usalama kwenye mipaka yetu ni shwari, ndani ya nchi yetu JWTZ kwa kushirikiana na vyombo vya wengine liko tayari kuwalinda wananchi na mali zao, wakati wote tupo tayari kukabiliana na matishio yoyote yanayojitokeza," amesema.