- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MASENETI WA MAREKANI WAMPA SIKU 6 TRUMP KUJIBU TUHUMA ZAKE
Baraza la Seneti nchini Marekani limepeleka wito kwa Rais wa nchi hiyo Donald Trump Alhamisi,hii ikimjulisha juu ya kesi yake na mashtaka yanayo mkabili dhidi yake na Ni lazima ajibu wito huo kwa maandishi mpaka ifikapo Jumamosi jioni mwezi huu.
Kesi ya Trump yakutaka kumuondoa madarakani imekuja wakati kuna mpasuko mkubwa wa kisiasa nchini na imekuja wakati Wademokrat, wakiwemo maseneta kadhaa, wakiwa wanagombea kinyang’anyiro cha nafasi ya urais dhidi yake katika uchaguzi wa rais unaokuja.
Taasisi inayofuatilia masuala ya serikali ilijumuisha Alhamisi kuwa Trump alivunja sheria ya matumizi ya serikali mwaka 2019 wakati alipositisha kwa muda matumizi ya dola za Marekani milioni 391 zilizokuwa zimepitishwa na bunge kwa ajili ya msaada wa kijeshi kwa Ukraine.
Kadhalika waangalizi hao wamesema Trump alishinikiza Kyiv kuanzisha uchunguzi ili kujinufaisha yeye mwenyewe. Uamuzi huo unajikita katika kiini cha kesi hiyo iliyofunguliwa dhidi ya kiongozi huyo wa Marekani.