Home | Terms & Conditions | Help

November 25, 2024, 1:46 pm

NEWS: MASAMAKI NA WENZAKE WAACHIWA HURU NA MAHAKAMA

Dar es salaam Mahakama kuu ya Tanzania leo imemuachia huru aliyekuwa Kamishna wa TRA, Tiagi Masamaki na Wenzake 5 awali Walishtakiwa kwa makosa ya uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya Tsh. Bilioni 12.7.

Washtakiwa wote wameachiwa huru baada ya upande wa mashtaka kusema kuwa DPP hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.

Pia walikuwepo Washtakiwa wengine waliokuwa katika kesi hiyo iliyotokana na sakata la makontena 329 ambapo ni Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru TRA, Habib Mponezya(45) na Meneja Msimamizi na Ufuatiliaji wa Forodha, Burton Mponezya(51).