- BREAKING NEWS: TANZANIA YAKANUSHA KUWASHIKILIA KINA DR SLAA NA MWAMBUKUZI
- BREAKING NEWS: RAIS WA MAPINDUZI WA NIGER AMTEUA WAZIRI MKUU MPYA
- BREAKING NEWS: SHILINGI YA KENYA YAPOROMOKA VIBAYA DHIDI YA DOLA
- BREAKING SEREKALI YA RWANDA YAKASIRISHWA NA UBELGIJI KUTOMUIDHINISHA BALOZI WAKE
- BREAKING NEWS: RAIS KIM AKUTANA NA WAZIRI WA ULINZI WA URUSI
NEWS: MAREKANI YAZINDUA MELI YA KIVITA YENYE THAMANI YA SHILINGI TRIL 26
Virginia:Rais wa Marekani Bw. Donald Trump siku ya Jumamosi alizindua meli ya kivita inayoitwa USSR Gerald R Ford, ambayo inatumia nguvu za kinyuklia na iliyogharimu karibu dola bilioni 13 kwa ujenzi wake kukamilika.
Uzinduzi huo ulifanyika katika mji wa Norfolk, Jimbo la Virginia, Marekani.
Trump alisema kuwa maadui wa Marekani watakuwa wakitetemeka watakapoiona meli hii ikikaribia walipo.
Ujenzi wa meli hiyo, ambayo pia ni ya kubeba ndege za kijeshi, ulianza mnamo mwaka wa 2009 na ulitarajiwa kukamilika mnamo mwaka wa 2015 kwa gharama ya dola bilioni 10.5.
Hata hivyo, ujenzi wake ulichukua muda mrefu na kugharimu kiasi kikubwa kuliko ilivyokadiriwa. Jeshi la majini lilisema kuwa kucheleweshwa huko, na ongezeko hilo la gharama, ni kutokana na mahitaji ya teknolojia ya kisasa ambayo imetumika kujenga meli hiyo.
USS Ford, imepewa jina la rais wa 38 wa Marekani, ambaye alihudumu kama Luteni kamanda wa jeshi la wanamaji wakati wa vita vya pili vya dunia. Alikuwa rais kati ya waka wa 1974 na 1977.